The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Asikitishwa na Jambo Hili – Video

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na ucheleweshaji wa vibali kwa wawekezaji wazawa na kuagiza mamlaka zinazohusika na uwekezaji kuacha kasumba ya kudharau wawekezaji wazawa.

Rais Samia amesema hayo leo Ijumaa, Desemba 3, 2021 wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha Raddy Fiber kilichopo wilaya ya Mkuranga huku akimpongeza amempongeza mwekezaji wa kiwanda hicho kwa uthubutu wake.

 

“Ndugu zangu mabibi na mabwana, serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa ufanyaji wa biashara na uwekezaji. Tunafahamu bila mchango wa sekta binafsi hatuwezi kuleta mageuzi makubwa ya uchumi wa nchi yetu.

 

“Ni muhimu tuendelee na jitihada za kutenga na kuendeleza maeneo maalumu ya kiuchumi, ili kurahisisha uwekezaji mkubwa katika sekta ya viwanda, kilimo, teknolojia na usafirishaji.

 

“Urasimu katika uwekezaji ni suala ambalo halina nafasi kwenye serikali hii, nilishaweka wazi kuwa nchi yetu inahitaji wawekezaji kuliko sisi tunavyowahitaji, sisi tunawahitaji zaidi kuliko wao wanavyohitaji Tanzania”. – Rais Samia.

 

“Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya uwekezaji ikijumuisha, barabara, viwanja vya ndege, reli, nishati, umeme, gesi na maji, kwa sababu Pwani ni mkoa wa viwanda tunaenda kuupa umuhimu pekee kwenye masuala ya maji, nishati na gesi.

“Kuna Watanzania wengi ambao sasa wameshatembea wameshaona, wamepata mitaji, wamejikusanya wanataka kurudi nyumbani kuwekeza na kutuletea faida, naomba muwakumbatie kwa majina yoyote watakayokuja nayo akija Samia Suluhu we mpe awekeze.

 

“Tuko katika wiki ya vuguvugu la sherehe ya miaka 60 ya uhuru wetu, na katika wiki hii tumeamua kuchagua baadhi ya viwanda na miradi mikubwa ya kitaifa kuifungua au kuiwekea majiwe ya msingi na leo tumeanza na kiwanda hiki,” amesema Rais Samia.

 

Leave A Reply