The House of Favourite Newspapers

Nec Yavipa Somo Vyama Vya Siasa

nec-2Mkurugenzi wa Nec, R.K Kailima akizungumza na waandishi wa habari.

nec-1Mkutano ukiendelea.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imevipa somo vyama vya siasa nchini huku pia ikitoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa iliyotolewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari juu ya malalamiko ya Chama Cha ACT-Wazalendo kulalamikia vyombo vya dola pamoja na watendaji wa umma kufanya vitendo vyenye mwelekeo wa kukipendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Nec, R.K Kailima, alisema kuwa katika taarifa ya chama hicho iliyotelewa jana,imeeleza kuwa Watendaji wa Halmashauri ya Geita waliwakusanya wazee katika Kata ya Nkome kuwapa vitambulisho vyao vya kupigia kura kwa lengo la kuwapatia huduma ya afya bure.

“ACT-Wazalendo wanalalamikia kitendo hichokwamba watendaji hao wanalengo la kuwahadaa wazee hao waweze kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Tume inapenda kuvikumbusha vyama vya siasa kwamba, kwa mujibu wa sehemu ya 5.3 ya maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 ambayo yalisainiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, serikali na vyama vya siasa, chama cha siasa au mgombea wa nafasi husika anayeamini kwamba maadili ya uchaguzi yamekiukwa awasilishe malalamiko yake katika kamati ya maadili ya ngazi husika.

“Hivyo tunakishauri Chama cha ACT-Wazalendo na vyama vingine vyenye wagombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani na vyenye wagombea wa udiwani katika uchaguzi mdogo kwenye kata 20 za Tanzania Bara,kutumia haki yao kuwasilisha malalamiko ya ukiukwaji wa maadili katika kamati husika,” alisemaKailima.

VilevileKailima alivitaka vyama vyote kwa kuzingatia sehemu ya 5.4 ya maadili ya uchaguzi kuvikumbusha kupeleka malalamiko yao ya ukiukwaji wa maadili ya uchaguzi kwenye kamati ya maadili ngazi ya kata ndani ya saa72 tangu ukiukwaji huo wa maadili ufanyike.

“Iwapo Chama cha siasa au mgombea hataridhika na maamuzi ya kamati ya maadili ngazi ya kata kwa kuzingatia sehemu ya 5.7(a) ya maadili ya uchaguzi awasilishe rufaa kwa msimamizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo ndani ya saa 24 tangu maamuzi ya kamati ya maadili ngazi ya kata kutolewa.

“Na kama chama cha siasa hakikuridhika na maamuzi ya kamati ya maadili ngazi ya jimbo,bado kwa kuzingatia sehemu ya 5.7 (b) na (c) wanayo fursa ya kuwasilisha rufaa yao katika kamati ya maadili ngazi ya Taifa au ngazi ya rufaa ambazo ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi,” alisema.

Aidha, Kailima ametoa wito kwa wananchi kwamba ni kosa chini ya kifungu cha 88 cha sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi,sura ya 343 na kifungu cha 100cha sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa,sura ya 292kumiliki kadi ya kupigia kura isiyokuwa yako na wananchi wasikubali kumpatia mtu yeyote kadi yao ya kupigia kura.

HABARI NA DENIS MTIMA/GPL

Comments are closed.