The House of Favourite Newspapers

Baada Ya Kuripoti Kombe La Mapinduzi, Mwandishi Afariki Dunia

amina-athumani-2

Amina Athumani enzi za Uhai wake.

MWANDISHI wa Habari za michezo wa magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani, Amina Athumani amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
amina-athumani-3Marehemu Amina Athuman (kulia) enzi za uhai wake akiwa na Mwandishi Andrew ChaleĀ 

Amina alikuwa visiwani Zanzibar kikazi, kuripoti michuano ya Kombe la Mapinduzi na Mwenyezi Mungu akamuongoza kuifanya kazi yake vizuri mwanzo hadi mwisho.amina-athumani-1Usiku wa kuamkia safari ya kurejea Dar es Salaam Jumamosi ndipo Amina aliyekuwa ana uja uzito wa miezi saba alipoanza kusumbuliwa kiafya. amina-athumani-4
Na inaelezwa asubuhi wakati anaelekea kwenye boti kurejea Dar es Salaam alianguka na kupelekwa hospitali binafsi, baadaye akahamishiwa Mnazi Mmoja. Siku hiyo hiyo Amina akajifungua mtoto ambaye kwa bahati mbaya alikwishafariki dunia.

Na usiku wa kuamkia leo naye amefariki pia. Taarifa zaidi za msiba huo zinatarajiwa baadaye kutoka kwa wahusika, hususan familia ya marehemu na waajiri wake, Uhuru Publication Limited. Mungu ampumzishe kwa amani Amina Athumani.

Comments are closed.