The House of Favourite Newspapers

Mrisho Mpoto Aungana na China Kutokomeza Ujangili Nchini

0

mpoto-1

Mwanamuziki wa Muziki wa Asili Bongo, Mrisho Mpoto ameipokea kwa furaha kauli ya Nchi ya China kutaka kukomesha biashara haramu ya meno ya tembo nchini. mpoto-2

Mpoto alionesha hiyo jana, Jumamosi katika matembezi ya amani yaliyoandaliwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing ambaye alisema kuwa nchi yake iko kwenye mkakati wa kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo na wanatarajia mwishoni mwa mwaka huu biashara hiyo itakuwa imeishakufa kabisa.

Aidha, Mpoto alipopewa nafasi ya kuzungumza kuhusu hatua ya China alisema kuwa ni hatua nzuri na itasaidia katika kupambana na kutokomeza ujangili wa meno ya tembo nchini.

 “Nimekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za wanyama hasa tembo ambao wamekuwa wakidhulumia pembe zao na majangili.

“Niwashukuru Ubalozi wa China kwa kunialika, nadhani wameona na wanatambua juhudi zangu katika kupinga ujangili nchini na kwingineko. Ilizoeleka kuwa China ndiyo kinara wa biashara hiyo lakini kwa kauli ya balozi wao, biashara hiyo inaenda kupotea kabisa.

Hata hivyo Mpoto aliongezea kuwa suala la kupinga ujangili nchini siyo la mtu mmoja, kila Mtanzania ana haki ya kulinda maliasili za nchi yake kwa ajili ya kizazi kijacho, na hivi karibuni anatarajia kuanzisha kampeni mbalimbali ambazo zitawafanya Watanzania kufichua majangili kwa kuwa ni watu ambao wanatoka katika jamii zao.

 Na:Gabriel Ng’osha/GPL

Leave A Reply