The House of Favourite Newspapers

Multichoice Yatoa Shukrani kwa Vyombo vya Habari Nchini

0

KAMPUNI ya Multichoice Tanzania inayouza Ving’amuzi vya DSTV, imevishukuru vyombo vyote vya habari vya hapa nchini kwa ushirikiano wao kwa muda wote wa mwaka 2016 uliomalizika hivi karibuni.

bendi-ya-sana-africa-music-ikitumbuiza

Bendi ya Sanaa Africa Music ikitumbuiza.

Shukurani hizo zimetolewa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Maharage Chande katika hafla fupi iliyofanyika jana Jumamosi kwenye Ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo, Chande alisema: “Sherehe hii ambayo awali tulitaka tuifanye kabla ya mwaka 2016 kwisha, ni maalumu kwa ajili ya kuwashukuru wanahabari wote pamoja na vyombo vya habari vya hapa nchini tulioshirikiana kwa mwaka mzima, kusema ukweli mmetubeba tena sana. bendi-ya-wamwituka-ikitumbuiza

Bendi ya Wamwituki ikitumbuiza.

img_0913

kutoka-kushoto-ni-meneja-uhusiano-wa-dstv-johnson-mshana-balozi-wa-maisha-magic-bongo-irene-paul-meneja-rasilimali-watu-wa-dstv-tike-mwakitwange-na-meneja-masoko-wa-dstv-alpha-mria

Kushoto ni Meneja wa Uhusiano wa DSTV Johnson….

maharage-chande-akisalimia-wageni-waalikwa

Maharage Chande akisalimina na Wageni Waalikwa.maharage-chande-akizungumza-na-wageni-waalikwa-pembeni-yake-ni-ofisa-uhusiano-wa-dstv-shumbana-walwa

Maharage Change akizungumza na wageni waalikwa.mkurugenzi-mtendaji-wa-multichoice-tanzania-maharage-chande

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania.

wilbert-molandi-akisalimiana-na-maharage-chande

Wilbert Molandi akisalimiana na Maharage Chande.

“Nakumbuka tangu Juni 15, mwaka jana wakati natambulishwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, vyombo vyote vya habari viliandika vizuri kwa kunikaribisha, na kuanzia hapo mpaka leo tumekuwa pamoja, matumaini yetu ni kwamba, mwaka huu utakuwa mzuri kwetu sote na kufanya mambo makubwa zaidi ya mwaka uliopita.”

Leave A Reply