The House of Favourite Newspapers

Joaquin “El Chapo” Akabidhiwa kwa Maafisa Marekani

joaquin-el-chapo-1Joaquin “El Chapo akiwa chini ya uandalizi wa maafisa wa Mexico.

MEXICO: Kiongozi wa genge la walanguzi wa mihadarati nchini Mexico Guzman Joaquin “El Chapo amehamishwa na kukabidhiwa kwa maafisa wa serikali nchini Marekani, serikali za nchi hizo mbili zilitangaza Alhamisi.

Aliwasili mjini New York kwa ndege kutoka Cuidad Juarez. Bwana Guzman, ambaye huen da akafungwa jela maisha nchini Marekani, amekuwa akisakwa na maafisa wa Marekani kwa tuhuma za ulanguzi wa dawa za kulevya. Anadaiwa kuingiza kiasi kikubwa sana cha dawa za kulevya nchini Marekani.

Kiongozi huyo wa genge la Sinaloa alikuwa anakabiliwa na maombi mawili ya kutaka apelekwe Marekani kujibu mashtaka – moja kutoka California na jingine Texas. Mwaka uliopita, alihamishiwa gereza la Ciudad Juarez, ambalo linapatikana maeneo ya mpakani karibu na mji wa El Paso katika jimbo la Texas.joaquin-el-chapo-2

Joaquin “El Chapo akiwa chini ya uandalizi wa maafisa wa Marekani.

Maafisa hata hivyo walikanusha tuhuma kwamba hatua hiyo ilikuwa kama maandilizi ya kumhamishia Marekani. Bw Guzman amekuwa akipigania kusalia Mexico lakini rufaa zake zilikataliwa. Amekuwa akilindwa vikali gerezani ikizingatiwa kwamba alikuwa ametoroka magereza mawili ya ulinzi mkali awali. Anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya dola mjini Brooklyn Ijumaa.

 

Chanzo BBC

Comments are closed.