The House of Favourite Newspapers

Sabby: Siwezi kutoka na Bella

sabby-2

“Sabby Angel”

MSANII wa filamu na Muziki wa Bongo Fleva, Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ amefungukia madai ya kutoka kimapenzi na msanii wa Muziki wa Dansi, Christian Bella kuwa hawezi kutoka naye na kwamba kazi za muziki ndizo zinamfanya kuweka mazoea naye. Christian Bella & Malaika Band - Amerudi

Christian Bella.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Sabby anayetikisa katika Tamthiliya ya Talaka pamoja na Ngoma ya Inahusu, alisema amekuwa akimposti Bella katika mitandao mbalimbali na kuwa naye karibu lengo likiwa kuonesha ‘alert’ ya kolabo naye mpya lakini wengi wameshindwa kuelewa na kumshambulia kukwa anabanjuka naye.

sabbyangel150115

“Sabby Angel”

“Bella ni kama my brother, siwezi kutoka naye na haitatokea. Kikubwa ambacho wengi hawaelewi ni kwamba nipo mbioni kuibuka na ngoma mpya niliyomshirikisha hivyo wasubiri waone siyo ‘kujudge’,” alisema Sabby.

Video: Madee Alivyowachana Mastaa Waliopotea kwenye Game

 

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.