The House of Favourite Newspapers

United Inamuonea Zlatan Ibrahimovic

man-u-zlatan

CHAMPIONI| MANCHESTER, England

UKWELI unabaki palepale kuwa Manchester United ina wakati mgumu sana msimu huu wa Ligi Kuu England. Timu hii chini ya kocha Jose Mourinho imeshindwa kuwania ubingwa na nafasi pekee ambayo inayo kwa sasa ni kupambana na kupata nafasi nne za juu.

Mourinho-Lampard-City-513573Mourinho.

Kama ikishindwa kumaliza kwenye nafasi hizo nne za juu litakuwa ni anguko lingine lakini kubwa sana chini ya kocha huyo raia wa Ureno. Mourinho alitua Manchester United na kuwahakikishia kuwa atatwaa ubingwa wa England msimu huu, lakini mambo yamekuwa magumu.

Timu hiyo imeweka makazi kwenye nafasi ya sita katika ligi hiyo maarufu duniani kwa sasa na takwimu mbalimbali hazionyeshi kama wanaweza kupanda kwa kasi kwenda nafasi za juu. Wikiendi iliyopita Wayne Rooney, aliifungia timu hiyo bao moja dakika za mwishoni kabisa na kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Stoke City.

zlatanibrahimovicmanchesterunitedvmanchesterlzqpkrnkrielZlatan Ibrahimovic

Lakini bado huu ulikuwa mchezo mwingine ambao umaliziaji mbovu uliendelea kuwasumbua kama ilivyo kwenye michezo mingine iliyopita. Manchester United haikuwa vibaya sana kwani ilifanikiwa kupiga mashuti 25 lakini bado walishindwa kuzitikisha nyavu za Stoke hadi Rooney alipoamka dakika za mwisho na kuwapa bao hilo kwa mkwaju wa faulo.

Kila mchezaji kwa wakati wake Juan Mata, Zlatan Ibrahimovic, Henrikh Mkhitaryan, Paul Pogba na Marcus Rashford, walipoteza nafasi ambazo unaweza kusema kuwa wangekuwa makini basi United walikuwa wanaibuka na ushindi mnono.

skysports-man-united-premier-league-zlatan-ibrahimovic_3825374“Tulifanya kila jambo vizuri isipokuwa mbele ya lango tu, tulikosa nafasi kadhaa, tulikuwa tunaweza kufunga bao kwenye kipindi cha kwanza au cha pili kutokana na nafasi zetu tulizopata,” alisema Mourinho.

Hata hivyo, huu ndiyo mchezo ambao United walionekana kupiga mashuti macha c h e zaidi langoni kwa t i m u pinzani. K i takwimu ni vigumu kuitoa Manchester United kwenye kasi ya ubingwa, lakini idadi ya pointi inaweza kukufanya ukakubali. Kabla ya kutoka sare na Liverpool, Manchester United walikuwa wameshinda michezo tisa mfululizo, lakini baada ya sare hiyo walifuatiwa na sare nyingine dhidi ya Stoke City na kumaliza kabisa ubabe wao.

man-u-zlatan4Kwenye michezo miwili walipoteza pointi nne ambazo zimewafanya sasa kuwa nyuma ya vinara Chelsea kwa tofauti ya pointi 14 ambazo ni nyingi sana kwa timu inayotaka ubingwa wa England Kamari ya Mourinho kumsajili, Zlatan Ibrahimovic imeonekana kukubali kwa kuwa mwenyewe tu ndiye amekuwa msaada mkubwa kwenye chati ya ufungaji wa timu hiyo.

Wakati Zlatan akiwa na mabao 14, mchezaji wa Manchester United anayefuata ni Juan Mata ambaye ana mabao manne. Hatari ni kwamba hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa United endapo tu Zlatan anaweza kukosekana uwanjani kwa kupewa kadi au kuumia.

Hii inaonyesha kuwa ni timu ambayo haiwezi kupambania ubingwa wa Ligi Kuu England kwa sasa ikiwa kwenye nafasi ya sita ambayo imedumu hapo kwa muda mrefu. United imeshafunga jumla ya mabao 33 yakiwa ni kumi nyuma ya timu inayoshika nafasi ya tano Manchester City.

Kama safu ya ulinzi, timu hiyo pamoja na kwamba imekuwa haina mabeki imara lakini imeruhusu mabao 21 ikiwa inashika nafasi ya tatu kati ya timu zile zilizofungwa mabao machache kwenye zile sita za juu.

“Nilikuwa nategemea kuna siku timu itakuja Old Trafford na kulala kwa mabao sita au saba, lakini bado naona mategemeo yangu hayajatimia mpaka, tunatakiwa kuendelea kupambana na kuona tutamalizia wapi msimu huu, ”alisema Mourinho.

Comments are closed.