JPM Aendesha Basi la Mwendokasi, Awaagiza Simbachawene na Mbarawa Kufikia Jioni Wampe Ripoti ya Makusanyo ya Mradi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop mara baada ya kutoka kukagua moja ya basi linalotumika katika utoaji huduma ya Usafiri wa Haraka (BRT)
Hapa nimekuwekea mlolongo wa matukio, hatua kwa hatua wakati Rais Magufuli alipozindua Rasmi Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka awamu ya kwanza, hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Gerezani vilivyopo maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam leo Jumatano, Januari 25, 2017 mchana.
#UzinduziwaBRT: Mgeni Rasmi, Rais Magufuli ameshawasili kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar (UDART) awamu ya kwanza inayofanyikia Kariakoo, Gerezani, Dar.
#UzinduziwaBRT: Mradi ukikamilika utaweza kujiendesha bila kuhitaji ruzuku kutoka serikalini. -Simbachawene
#UzinduziwaBRT: Live Kutoka Kariakoo, JPM Akizindua Rasmi wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi DSM.
#UzinduziwaBRT: Endapo mradi huu utakamilika ipasavyo, UDART itakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 450,000 kwa siku.- Waziri Simbachawene.
#UzinduziwaBRT Madhumuni ya Mradi huu ni kushusha kiwango cha nauli ili Watanzania waweze kutumia usafiri huu. Waziri Simbachawene.
#UzinduziwaBRT: Kiwango cha nauli kushuka Mradi kuweza kujiendesha bila kuhitaji ruzuku kutoka serikalini. – Waziri Simbachawene.
#UzinduziwaBRT: Serikali inamiliki asilimia 49 za hisa wakati Kampuni ya Simon Group inamiliki 51 za UDA. – Waziri Simbachawene.
#UzinduziwaBRT AWAMU ZA UJENZI WA UDART
Awamu ya 1- Kimara Kivukoni, Magomeni hadi Moroko, Kariakoo
Awamu ya 2: Barabara ya Kilwa hadi Gerezani na Mbagala Rangi Tatu, fly overs kati ya Chang’ombe na Uhasibu.
Awamu ya 3- Barabara ya Nyerere, Uhuru, Bibi Titi na Azikiwe katikati ya jiji la Dar es Salaam hadi Gongo la Mboto.
Awamu ya 4. Bibi Titi, Sam Nujoma na Nyerere.
Awamu ya 5. Barabara ya Mandela.
Awamu ya 6. Barabara ya Mwai Kibaki.- Amesema Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa.
#UzinduziwaBRT: Rais Magufuli amesema mkandarasi wa kwanza wa Mradi wa Mwendokasi alikuwa Mchina, alishindwa akatumbuliwa akaondoka ndipo akaletwa Strasburg wa Ujerumani.
#UzinduziwaBRT: Rais Magufuli aiagiza Wizara ya Ujenzi kushughulikia changamoto iliyoko Makutano ya Barabara Ubungo Mataa ili kufanikisha Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka.
#UzinduziwaBRT: Rais Magufuli awaagiza Mawaziri George Simbachawene wa TAMISEMI na Prof. Makame Mbarawa wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi pamoja na wasimamizi wa mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dara, kufikia leo jioni wampe ripoti inayoonesha kiasi cha fedha iliyopatikana kama faida kwenye mradi huo.
‘Mawaziri mmetoa taarifa nzuri lakini mmeninyima raha kwa kotonipa taarifa ya pesa mlizotengeneza kutokana na mradi huu’
‘Nilitaka nijue kama mradi umetengeneza faida basi ningetoa maagizo Kimara pajengwe kituo kikubwa cha maegesho ya magari’
‘Nawaagiza kufikia leo jioni muwe mmenipatia ripoti ya kiasi cha faida kilichopatikana tangu mradi huu uanze ili nijue kama kuna faida au hasara, kama ripoti mnazo mnipe hapa sasa hivi.’ Alisema Rais Magufuli.
#UzinduziwaBRT: Rais Magufuli amependekeza kujengwa kwa kituo kikubwa cha maegesho ya magari ya daradala na madogo madogo eneo la Kimara ili kuvutia watu ambao wakishuka kwenye magari yao binafsi ama daladala wapande ya mwendokasi, au wakishuka mabasi ya mwendokasi iwe rahisi kupanda daladala au magari yao binafsi.
‘Wapo watu wanatoka na magari yao wanapofika Kimara wanataka watumie mabasi ya haraka lazima kuwe na eneo la parking ya magari’
‘Tumepanga kujenga barabara za juu kwenye makutano ya barabara DSM na kujenga daraja litakaloanzia Coco Beach mpaka Hospitali ya Aga Khan.”
“Miradi ya mabasi ya haraka ktk Afrika ipo Nigeria na Afrika Kusini lakini miradi hiyo sio mikubwa kama huu wa Tanzania.” Alisema Rais Magufuli
#UzinduziwaBRT: Rais Magufuli awaagiza vikosi vya Usalama Barabarani kuwashughulikia wanaoingiza magari kwenye njia za mwendokasi kwani wanavunja sheria za nchi. Ameagiza wakamatwe na kupelekwa vituo vya polisi ama kung’oa mataili kwenye magari yao ili liwe fundisho kwao na kwa wengine.
‘Trafiki mkiona pikipiki, gari linatumia barabara hizi za mwendokasi yashikeni pelekeni kituo cha polisi, yatoeni matairi ili wajifunze’
“Saa nyingine ukitumia sheria tu watu hawajifunzi lazima mtumie nguvu za ziada ili waziogope hizo barabara za mwendokasi.” Alisema Rais Magufuli.
#UzinduziwaBRT: Rais Magufuli amezindua Rasmi Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka, awamu ya kwanza katika Viwanja vya Gerezani vilivyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
#UzinduziwaBRT: Rais Magufuli amezindua rasmi Miundo Mbinu ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka, awamu ya kwanza katika Viwanja vya Gerezani, Kariakoo jijini Dar.
#UzinduziwaBRT: Rais Magufuli ameendesha moja ya mabasi ya mwendokasi wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi, Viwanja vya Gerezani, Kariakoo jijini Dar.
#UzinduziwaBRT: Akizungumza kuhusu utekelezwaji na uboreshwaji wa Mradi wa Mabasi Yendayo Haraka jijini Dar, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema ametoa agizo kwa wamachinga wote wanaofanya kazi zao kandokando ya barabara za mabasi ya mwendokasi waondoke wenyewe kulekea kwenye maeneo waliyotengewa ambayo moja wapo ni Mtaa wa Lumumba kabla ya Manispaa yake haijachukua hatua za kuwaondoa kwa nguvu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakati Msanii Mrisho Mpoto alipokuwa akitumbuiza.
#UzinduziwaBRT: Naye Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene ameongeza kuwa wmachinga wanaofanya biashara zao kwenye njia za waenda kwa miguu waondoke mara moja kwani wanavunja sheria na kusababisha madhara na hata watembea kwa miguu kugongwa na magari na kufa.
Comments are closed.