The House of Favourite Newspapers

Joh Makina vs Fid Q: Huyu Anatafuta Hela, Yule Anatafuta Heshima

fid-q

Fid Q.

WAKATI unaanza kuingia Bongo, muziki wa Hip Hop ulikuwa ukitafsiriwa tofauti sana ukilinganisha na aina nyingine ya muziki. Wasanii wa Hip Hop walionekana wahuni, wavuta bangi, wasio na ‘future’ na ambao hawawezi kutusua kwenye gemu la muziki wa Bongo.

Wasanii kama Madee, walifikia hatua ya kuchana hadharani kwamba Hip Hop hailipi, bora kubana pua. Hali hiyo ilisababisha wasanii wengi waliokuwa wakifanya Hip Hop, taratibu kuanza kubadilisha uelekeo, wakaanza kuimba nyimbo laini na kweli Hip Hop ikaonekana kama inaelekea kaburini.

Hata hivyo, licha ya wengi kuikacha Hip Hop, bado wachache waliendelea kukaza kamba na hapa unawazungumzia watu kama Fareed Kubanda ‘Fid Q’ ukipenda muite Ngosha The Don, John Simon ‘Joh Makini’, Chindo Man na kruu yake ya Watengwa, Profesa Jay, MwanaFA, Nako 2 Nako Soldiers, Danny Msimamo, Sugu na wakongwe wengine kabla ya baadaye kuibuka kizazi kingine cha wasanii kama Roma Mkatoliki, Stamina, Young Killer ‘Msodoki’, Darassa na wengine kibao.

Licha awali kuonesha kwamba wanaisimamia msingi ya Hip Hop, ukiwasikiliza kwa makini wasanii wote hao, utagundua kwamba kadiri muda unavyosonga mbele, wengi wameanza kubadilika, kutoka kwenye ile Hip Hop Hard Core na kwenda kwenye mchanganyiko ambao kwa jina lolote utakalouita, unaangukia kwenye Bongo Fleva.

Joh-makini.jpg

Joh Makini.

Hapa ndipo inapoibuka tofauti kati ya wakali wawili ambao kwa kipindi kirefu, walikuwa wakichuana kwenye gemu, kiasi cha kuwagawa mashabiki wao, Fid Q na Joh Makini.

 

Ipo wazi kwamba wakati Fid Q ana-hit na ngoma zake kama Chagua Moja, Mwanza Mwanza, Agosti 13, Huyu na Yule, Neno, Ni Hayo Tu na nyingine kibao, mpinzani wake mkubwa alikuwa ni Joh Makini, Mwamba wa Kaskazini.

Kwa upande wake, Joh alikuwa akikimbiza na ngoma zake kama Ufalme, Ni Zamu Yangu, Popote Chochote, Stimu Zimelipiwa na nyingine kibao, gumzo kubwa kwa mashabiki wa Hip Hop likawa ni miamba hiyo miwili, mmoja akitokea Kanda ya Ziwa kwa maana ya Mwanza na mwingine akitokea Kanda ya Kaskazini, kwa maana ya Chuga (Arusha).

Ukweli ambao hata kama wewe ni mbishi, leo utakubaliana nao, ni kwamba baada ya miaka mingi, huwezi tena kuwasimamisha Fid Q na Joh Makini na kuwalinganisha kwa chochote kile. Muziki wanaofanya haufanani tena, mashabiki wao hawafanani tena, video zao hazifanani tena na hata mafanikio yao nje ya gemu, hayafanani tena.

Kilichowatofautisha, ni kwamba Fid Q aliamua kusimamia falsafa ngumu kama za kina Karl Max, akaendelea kufanya Hip Hop ngumu bila kujali kwamba tayari soko lilishabadilika na Wabongo hawakuwa wakivutiwa kusikiliza mistari migumu tena bali wanataka ngoma za kuruka na ku-party!

Joh Makini yeye alikuwa mjanja, akabadilika kufuata upepo, taratibu akaanza kuhama kutoka kwenye Hip Hop ngumu hadi kwenye muziki unaopendwa, kwa lengo la kusaka mkwanja na kweli akafanikiwa. Video zake nazo zikabadilika na kuanza kufukuzia ubora wa kimataifa, naye akawa anaenda ku-shoot kwa akina God Father na mabadiliko yanaonekana wazi.

Kupanga ni kuchagua, Fid Q aliamua kuchagua heshima na kweli hadi sasa anaendelea kubaki na heshima yake ya kuwa msanii anayesimamia misingi ya Hip Hop kwelikweli. Tazama hata kwenye ngoma yake ya Roho, ameimba mapenzi kwa hisia lakini bado anasimamia Hip Hop. Naweza kusema kwamba Fid Q ameweza kusimamisha heshima katika Hip Hop, bila kujali kwamba anaishi maisha gani wala anatembelea usafiri gani! Pongezi kwake.

Kwa upande wa Joh Makini, naye kwa kuwa aliamua kuchagua kutafuta mkwanja kwa namna yoyote, akiwa chini ya Kampuni ya Weusi, amefanikiwa kupiga mkwanja na kujitangaza hadi nje ya mipaka ya Tanzania. Amefanikiwa kupata mashabiki ambao awali hawakuwa wakimkubali kwa sababu ya ugumu wa mashairi yake

Save

Comments are closed.