The House of Favourite Newspapers

Saida Karoli: Bora Kukaanga Vitumbua au Maandazi Kuliko Kuimba

Saida Karoli

KUPITIA kipindi cha Take One  cha Clouds TV, msanii maarufu wa nyimbo za asili nchini, Saida Karoli amefunguka jinsi alivyodhurumiwa kazi zake za sanaa kwa kutojua kusoma na kuandika.

Mtangazaji na mwendeshaji wa kipindi hicho, Zamaradi Mketema, ‘Zama’ alimuhoji mwimbaji huyo ambapo alikiri kuwa hana haki kwenye nyimbo zake kutokana na mikataba aliyosainishwa na Meneja wake sababu na yeye hakuwa anajua kusoma na kuandika na akadai zaidi ya album tano hana haki nazo na meneja wake wa zamani ndio mwenye haki nazo.

Picha katika Video ya Salome Wimbo wa Saida Karoli uliorudiwa na Diamond Platnumz

Saida aliendelea kufunguka hadi katika wimbo wa Salome ambao Diamond Platnumz aliurudia, alisema ana hesabu kama alitoa bure kwani hata fedha aliyopewa ni kidogo na haifai kuongelea.

”Siwezi kulalamika hata kidogo, mara nyingi naulizwa nasema sina tatizo, sina haki na zile nyimbo maana yeye ndio alinipa mikataba na yeye ndio alinitengenezea, hata hii ya Diamond naweza nikasema ikawa mbaya zaidi maana fedha niliyoipata siyo ya kuongelea, kwahiyo mimi najiona nimetoa bure

”Waandishi kila siku wanakuwa wananiuliza nawambia nimempa Diamond nyimbo bure na nimetoa kwa moyo mmoja kweli, roho yangu moja

Saida Karoli

“Meneja wa zamani aliniuliza nyimbo yako inatakiwa kutumika lakini nipe idhini yako japo ni nyimbo zangu zote lakini sikuwa na haki licha ya kuwa sauti yangu imesikika kule, mimi nilimjibu nimeshakata tamaa na kuimba naona muziki kwangu hauna faida na thamani bora kuwa hata mkaanga vitumbua au maandazi kuliko kuimba

”Nilikuwa na mpango wa kurudi kijijini nyumbani nikae mtu akihitaji show atanikuta kijijini lakini meneja akanambia hapana, alisema nyimbo tumpe Diamond kwa sababu itaniinua na kunipa moyo na kuniamsha upya kama mtu aliyekufa

Aidha kwa sasa Saida yupo Dar na amekuja rasmi kwa ajili ya kufanya muziki upya kama zamani na yupo tayari kufanya kazi na wasanii wa sasa kama vile Daimond mwenyewe, Darasa na wasanii wengine.

Salum Milongo/GPL

Comments are closed.