The House of Favourite Newspapers

EXCLUSIVE: Global TV Online Yatunukiwa ‘Silver Play Button’ Na YouTube – (Pichaz)

 

CHANNEL ya Global TV Online inayokimbiza Afrika Mashariki kwa stori za Burudani, Habari za Jamii, Kitaifa, Kimataifa, Siasa na Michezo, imetunukiwa ‘Silver Play Button’ na wamiliki wa mtandao maarufu wa video duniani YouTube.

Huwa ni utamaduni wa YouTube kutambua channel zote zinazoleta impact kupitia videos mbalimbali zinazowekwa kwenye mtandao huo. Video hizi zinaweza kuwa za kitu chohote kinachofurahisha, kuelimisha, na kuiburudhisha jamii nzima ya wana-YouTube ambao ni watazamaji kutoka kila pembe ya dunia.

Kwenye list ya zile channel zinazoleta impact hiyo, channel yako pendwa ya Global TV Online imepata bahati ya kuwa miongoni mwa channel hizo, hivyo kufanikiwa kujinyakulia zawadi ya ‘YouTube Silver Play Button’ kutoka Makao Makuu ya YouTube, San Bruno, California, nchini Marekani kwa kujikusanyia Subscribers (watazamaji waliojiunga) zaidi ya 153,000.

Tuzo hiyo imewasilishwa na kukabidhiwa leo Machi 16, 2017 kwa Timu ya Global TV Online kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga, Mwenge Dar es Salaam na Clement Rapudo Director wa Kampuni ya Ngomma Vas Ltd. kutoka nchini Kenya.

Cheki picha za YouTube Silver Play Button hapa chini.

Silver Play Button ya YouTube ya Global TV Online

YouTube hutoa  Play Buttons hizi kwa stage nne ambazo ni:

  • The Silver Play Button, kwa channel zilizofikia subscribers 100,000.
  • The Gold Play Button, kwa channel zilizofikia subscribers 1,000,000.
  • The Diamond Play Button, kwa channel zilizofikia subscribers 10,000,000.
  • The Ruby Play Button, kwa channel zilizofikia subscribers 50,000,000.

Timu ya Global TV Online wakipokea Silver Play Button hiyo kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Ngomma Vas Ltd, Clement Rapudo (wa nne kushoto mwenye miwani na Tshirt nyeusi).

 

Comments are closed.