The House of Favourite Newspapers

Davido: Nampenda Sophia Kinoma!

LICHA ya hivi karibuni kuweka hadharani kuwa anatarajia kupata mtoto wa pili kwa demu wake mpya mwenye asili ya Marekani, Mandy, staa wa muziki kutoka Naija, David Adeleke ‘Davido’ amefunguka ya moyoni kuwa bado anampenda kinoma mzazi mwenzake wa kwanza aitwaye Sophia Momodu aliyezaa naye mtoto mmoja, Imade.

Davido aliyasema hayo alipofanyiwa mahojiano na redio moja nchini Nigeria kuwa, hawezi kumsahau wala kumtupa mzazi mwenzake kwa kuwa amezaa naye.

“Nampenda mzazi mwenzangu, haahaa, Sophia sikia hii popote ulipo!” Davido na Mandy walianzisha uhusiano Atlanta, Georgia huko Marekani na hadi sasa demu huyo ameshakanyaga Jiji la Lagos anapoishi Davido mara moja yaani Desemba 2016.

Comments are closed.