The House of Favourite Newspapers

Sirro: Tumemkamata Mwizi Akiiba Mafuta ya Ndege ya ATCL

KAMISHNA wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa mnamo Machi 17 mwaka huu kwenye hanga la Kampuni ya ndege Tanzania ATCL uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Polisi kwa kishirikiana na maofisa wa uwanja huo wamemkamata Iddy Juma Nyangasa(42) ambaye alikuwa mlinzi wa Kampuni ya Moku Security akiiba mafuta ya ndege lita 38.

Akizungumza leo na waandishi wa Habari jijini Dar, Sirro amesema kuwa mafuta yaliyokuwa yakiibwa kwenye ndege yenye namba za usajili 5H_MWF aina ya DASH 8_Q 300 Mali ya Kampuni ya ndege ya Tanzania  iliyokuwa kwenye hanga hilo kwa ajili ya matengenezo.

Alifafanua kuwa hata hivyo baada ya ukaguzi wa kina kutoka kwa wahandisi wa shirika hilo ilibainika kuwa jumla ya lita 220 ndizo zilizoibiwa toka katika ndege hiyo.

Aliongeza kuwa katika mtandao huo wa wizi wa mafuta unahusisha Askari Polisi wa kikosi cja Anga ambao aliwataja kwa majina ya F 8419 CPL Bahati na F 9901 PC Benaus ambao tayari wamekamatwa kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo na mara tu uchunguzi ukikamilika watuhumiwa wote watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Comments are closed.