The House of Favourite Newspapers

Hazard Nje Siku 15

KIUNGO wa Chelsea, Eden Hazard ameumia na hivyo atakaa nje kwa zaidi ya siku 10 hali iliyomfanya ashindwe kujiunga na timu yake ya taifa ya Ubelgiji.

Kocha wa timu hiyo ya taifa Roberto Martinez, amesema mchezaji huyo ana majeraha ya nyama za paja na hataweza kujiunga na timu hiyo ya taifa ambayo itacheza michezo miwili dhidi ya Ugiriki na Urusi.
Imeelezwa kuwa mbali na kushindwa kujiunga na timu hiyo pia atashindwa kuitumikia klabu yake kwenye
mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace.

Kiungo huyo amekuwa moto mkali msimu huu, alishindwa kuichezea Chelsea kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu England dhidi ya Stoke City. “Eden aliumia hata kabla ya mchezo dhidi ya Stoke na kwa hali ya majeraha yake yalivyo atakaa nje kwa zaidi ya siku 15, anaonekana kuwa na jeraha kubwa kidogo. “Naamini hata yeye hawezi kufurahia hali hii aliyonayo bado inaonekana anaweza kukosa hata mchezo mmoja wa ligi unaokuja,” alisema kocha huyo.

Hazard alikuwa anatarajiwa kuwa nahodha kwenye michezo hiyo ya kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Na Mwandishi/ CHAMPIONI/GPL

Comments are closed.