The House of Favourite Newspapers

MACHOZI: Nimepelekwa Ulaya na mwanamke wa Kizungu?

 

Hussein Machozi.

Na GABRIEL NG`OSHA| GAZETI LA AMANI| MAKALA

UNAMKUMBUKA Mbongo-Fleva, Hussein Machozi? Jamaa aliwahi kutamba na Ngoma za Kafia Gheto, Utaipenda na nyingine kibao. Machozi kwa sasa yuko barani Ulaya nchini Italia. Anajishughulisha na mchezo wa kwenye barafu. Kibongobongo kuna tetesi kuwa alipelekwa nchini humo na mwanamke wa Kizungu ambaye ana uhusiano naye wa kimapenzi.

Ili kupata undani wa ishu hiyo, Over Ze Weekend ilimtafuta Machozi kwa njia ya simu ambapo alifunguka kuhusu maisha yake ya ughaibuni; Machozi umepotea sana kwenye gemu, nini tatizo? Hakuna kilichonipoteza zaidi ya kuwa bize na mambo yangu mengine.

Hussein Machozi akifanya usafi wa miguu huko Ulaya.

Ni kweli wadau wa muziki wanawapoteza au muda wenu unakuwa umeisha tu? Kwa upande wangu sijapotea na soon mashabiki wangu wataniona. Ni kweli kwamba wadau huwa wanachangia sana kuwapoteza wasanii wengi huwa wanafanya biashara zao za kitapeli wakitumia mgongo wa wasanii.

Machozi na anayedaiwa kuwa Mzungu wake (Mpenzi wake)

NINI KIPYA KWA SASA KWENYE SANAA YAKO?

Nakuja na ngoma mpya ambayo itaonesha upya wa Hussein Machozi. Sitaki kuongea sana kwani raia ndiyo wataongea.

NGOMA YAKO MPYA INAITWAJE?

Wimbo wangu mpya unakwenda kwa jina la Nipe Sikuachi.

KWENYE NGOMA ZAKO,

IPI HUWA INAKUBAMBA NA HUWEZI KUISAHAU NA KWA NINI? Ngoma ya Kafia Gheto siwezi kuisahau. Hii ni kwa sababu ilinipa nguvu katika maisha yangu. Ilinipa mama Zakia (mke wake) ambaye ni furaha, amani na jicho langu.

UNA MTOTO AU WATOTO?

Nina mtoto mmoja tu, anaitwa Zakia.

KUNA KIPINDI ULIKUWA NA BIFU NA MKEO AMBAYE MLIACHANA, LILIISHAJE?

Mke wangu ni mama Zakia ambaye hadi leo niko naye. Yupo Tanzania na hatujawahi kuachana.

NINI KILIKUPELEKA ITALIA?

Kilichonileta Italia ni masomo.

MCHEZO WA KWENYE BARAFU UMEJIFUNZIA WAPI NA KWA MUDA GANI?

Nimejifunza hukuhuku (Italia). Nilitumia wiki moja tu lakini nikawa ‘kisu’ balaa hadi mwalimu aliyekuwa ananifundisha akadata.

UMEKUNUFAISHA NINI?

Kwa kuwa sina muda mrefu tangu nimeanza kuufanya, sijapata mafanikio makubwa ila naamini utanifikisha sehemu.

NI KWELI ULIPELEKWA ITALIA NA MWANAMKE WA KIZUNGU?

Sina na wala sijaletwa na mwanamke wa Kizungu bali ni akili zangu na kujiongeza kila kukicha.

NDIYO KUSEMA UMEHAMA KABISA BONGO?

Mimi ni raia wa Tanzania, siwezi kuhama nyumbani, nitarudi na mishe zitaendelea kama kawa.

NINI KIGUMU HUKO?

Kigumu ni vyakula vyao, havifanani na vya Bongo, nikisema nikale mgahawani, kote wanapika kitimoto na mimi ni Muislam, hivyo inanibidi nijipikie mwenyewe ingawa ni vigumu kupata kitu cha kupika ninachokijua, ni tabu tu!

UMECHUKUA MUDA GANI KUJUA KIITALIANO?

Ni muda mchache sana, kama miezi mitatu hivi nikawa ninakitwanga.

VIPI KUHUSU MKEO NDIYO UMEMUACHA BAADA YA KUPANDA MTASHA?

Siwezi kumuacha mama Zakia wangu hata kama ningekuwa na Mzungu, nitakufa naye.

LINI UNATEGEMA KUFUNGA NDOA RASMI?

Muda wa ndoa ukifika watu watajua tu.

KWA NINI MUZIKI WA BONGO HAUWANUFAISHI WASANII?

Una bonge la kirusi na hakiwezi kufa leo wala kesho. Wanamuziki wote wanakijua na wanakiogopa, mbaya zaidi ukikugusa tu unapotea mzimamzima.

ULIKUWA NA KIPAJI CHA MPIRA, JE, KIMEISHIA WAPI?

Kipaji huwa hakifi, ni kujipanga tu….wanasema mpira ukiujua umeujua tu yaani ni kama baiskeli.

 

Comments are closed.