The House of Favourite Newspapers

Kevin Durant Atoa Matumaini ya Kurejea Mapema

Kevin Durant.

LICHA ya kuonekana kuwa anaweza kuwa nje ya uwanja muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi, imeelezwa kuwa Kevin Durant anaweza kurejea uwanjani kabla msimu huu haujafikia mwisho.

Durant ambaye anaichezea Golden State Warriors, aliumia goti na hajacheza tangu Februari 28, mwaka huu na ikaelezwa kuwa jeraha lake litaangaliwa na kutolewa majibu wiki nne baadaye .

Jumanne ya wiki hii alionekana akitembea vizuri wakati timu yake ilipokuwa ikicheza dhidi ya Dallas katika ligi ya kikapu ya NBA. Wastani wa Durant kabla ya kuumia ni pointi 25.3, rebounds 8.2 na asisti 4.8 kwa msimu huu.

 

Comments are closed.