The House of Favourite Newspapers

Kisa Ujauzito Galatoni Ampiga Chini Linah

Esterina Sanga ‘Linah’.

Na GABRIEL NG`OSHA| GAZETI LA UWAZI| SHOWBIZ

MWANAMUZIKI Ahmed Sadala a.k.a Galatone aliyewahi kutamba katika Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva na Wimbo wa Samaki amefunguka kuwa suala la mwanadada mrembo na Mwanamuziki Esterina Sanga ‘Linah’ kupata ujauzito limemkatisha tamaa kiasi cha kuamua kupiga chini harakati zake za kumnasa.

Linah.

Akichonga na Uwazi Showbiz, Galatone alisema kuwa Linah alikuwa ni mwanamke wa ndoto zake na alikuwa amepanga kuzianza harakati za kummendea hivi karibuni lakini baada ya kugundua kuwa ni mjamzito imebidi kujiweka pembeni na kumfi kiria mwanamke mwingine atakayempenda kama Linah.

Ahmed Sadala ‘Galatone’.
Linah

“Najilaumu mwenyewe kwa .uzembe wangu wa kusubiri kujitosa kwake nikiamini muda ulikuwa haujafi ka, lakini sina namna inabidi tu kujiweka pembeni maana tayari wajanja wamemuwahi na si rahisi kunikubalia na kumuacha anayekwenda kuwa baba wa mtoto wake,” alimaliza Galatone

Comments are closed.