The House of Favourite Newspapers

Khloe Kardashian Apania Kuolewa na Tristan

0
Khloe Kardashian na Tristan Thompson.

HOST wa Kipindi cha Keeping Up With The Kardashians (KUWTK), Khloe Kardashian ameibuka na kusema kuwa, hata iweje lazima ahakikishe ameolewa na mpenzi wake wa sasa, Tristan Thompson ingawa bado wanachunguzana.

Akizungumza katika mahojiano yake na Jarida la ES mara baada ya kuulizwa swali juu ya uhusiano wake na staa huyo wa NBA, alijibu;

“Ninatamani kuwa na familia.” Na alipoulizwa iwapo atachumbiwa na mwanaume huyo atakubali au la, alijibu harakaharaka ndiyo na kuongeza kuwa lazima atafanya hivyo licha ya kuwa ana mtoto.

“Tristan tayari ni baba na ana majukumu lakini pia nataka na mimi kumzalia ili niwe mama wa watoto wake, sina presha sana najua muda utafi ka,” alisema Khloe aliyewahi kuwa na uhusiano na staa mwingine wa NBA, Lamar Odom.

 

Leave A Reply