Serengeti Boys kuwavaa Gabon kesho

Wachezaji wa timu ya Serengeti Boys.

Ibrahim Mussa | Championi Ijumaa | Habari
TIMU ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya miaka 17, Serengeti Boys, kesho Jumamosi inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gabon katika Viwanja vya Shirikisho la Soka Morocco (FRMF) nchini Morocco.
Serengeti Boys inajiandaa na fainali za mataifa Afrika kwa vijana zinazotarajiwa kuanza Mei 14, mwaka huu nchini Gabon ambapo wamepangwa Kundi B sambamba na Niger, Angola na Ethiopia.


Akizungumza na Championi Ijumaa moja kwa moja kutoka kambini nchini Morocco, Shime alisema lengo la mchezo huo ni kuangalia mapungufu ya kikosi chake kabla ya kulekea nchini Gabon tayari kwa mashindano hayo.
“Tunashukuru maandalizi yapo vizuri na kila kitu kipo sawa, vijana wako na ari kubwa kabisa na wako tayari kwa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Gabon ambao ndiyo wenyeji wa michuano hiyo, naamini itatusaidia kujua aina ya timu tunazoenda kucheza nazo, hivyo kwetu ni jambo zuri.
“Hii mechi itasaidia kutambua mapungufu ya wachezaji wangu kabla ya kurudiana nao Aprili 25 kwa sababu baada ya kucheza na Ghana nyumbani hatukucheza mchezo wowote,” alisema Shime.

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment