The House of Favourite Newspapers

Ninja: Nampoteza Emmanuel Okwi Uwanjani

0
Beki wa kati Abdallah Haji Shaibu maarufu kama Ninja kutoka Klabu ya Taifa Jang’ombe akiweka wimo Jangwani.

YANGA imemsajili beki wa kati Abdallah Haji Shaibu maarufu kama Ninja kutoka Klabu ya Taifa Jang’ombe ya visiwani Zanzibar, tayari beki huyo amechimba mkwara kwamba ana uwezo wa kumzuia mshambuliaji Emmanuel Okwi anayetarajiwa kusaini Simba muda wowote.

Mshambuliaji Emmanuel Okwi anayetarajiwa kusaini Simba muda wowote.

Ninja anatajwa kuwa mrithi wa nahodha w a timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anayecheza pia beki ya kati. Ninja alianzia soka Liver Nile FC mwaka 2008 halafu akaenda Lui Vaico alipokutana na Kocha Ally Wazir, na mwaka 2009 alijiunga na Junior FC.

Mwaka 2011 alijiunga na Yatosha kisha akaanza kucheza ligi za madaraja ya chini kisha akajiunga na Bento, ambako hakudumu kwani alijiunga na timu ya vijana ya Mtibwa Sugar. Mwaka 2014 alirejea Zanzibar alijiunga na Taifa Jang’ombe wakati huo ikiwa daraja la pili, akaipandisha daraja hadi daraja la kwanza halafu Ligi Kuu Zanzibar na mwaka huu amejiunga na Yanga. Championi Jumamosi limefanya mahojiano na beki huyo ambaye ni maarufu visiwani Zanzibar, na hii ni sehemu ya mahojiano;

HIVI YANGA WALIKUONA WAPI?

“Ilikuwa k a t i k a Kombe l a Mapinduzi mwaka huu nikiwa na timu ya Taifa Jang’ombe, nilizungumza nao kawaida tu katika siku za mwanzo lakini sana viongozi wangu wakaniambia Yanga wananitaka. “Meneja wangu akaongea na Yanga kisha tukakubaliana maslahi, nami sasa ni mchezaji wa Yanga.

YANGA NI TIMU KUBWA, UMEJIPANGA VIPI KWA USHINDANI WA NAFASI?

“Nimejipanga vizuri kwa sababu lazima nipambane ili niweze kucheza, nategemea uwezo wa Mungu kuweza kufanikisha hilo pamoja na juhudi zangu ambazo nitazionyesha. “Si kazi rahisi kucheza kikosi cha kwanza kwani wapo Cannavaro (Nadir

Haroub), Y o n d a n i (Kelvin) na Bossou (Vincent) hata Dante (Andrew Vincent), hapa natakiwa kupambana ila siogopi “Siwahofii, naamini juhudi zangu zitanipa nafasi kikosi cha kwanza, pia ni lazima nishirikiane nao ili niwe bora zaidi.

KWA NINI UNAITWA NINJA?

“Kuna shabiki mmoja ndiye aliyeanzisha jina la Ninja kabla sijajiunga na Taifa Jang’ombe, nilikuwa nacheza sana mechi za ndondo na nilikuwa nafanya kazi kubwa ya kukaba kwa nguvu. “Uchezaji wangu huo ndiyo ukamfanya shabiki huyo aniite Ninja, nilipojiunga na Taifa Jang’ombe jina likawa kubwa hadi leo wananiita hivyo.

NJE YA SOKA UNAPENDELEA KUFANYA NINI? “Nje ya soka huwa napenda sana kupiga dufu katika madrasa yetu ya Manzi ambayo nimesoma, muda ambao sipo uwanjani huwa nipo hapo madrasa.

UMEJIPANGA VIPI KUISHI JIJINI DAR ES SALAAM KWENYE VURUGU ZA KILA AINA?

“Mimi najitambua pia najua vitu vya Dar es Salaam, nimejipanga kuepuka changamoto zote, nimeambiwa kuna vishawishi vingi kwamba nitafuatwa na wasichana wa kila aina. “Nitakuwa makini na mambo hayo ili yasiweze kunitoa mchezoni hivyo nipo makini na maisha ya Dar es Salaam.

UNAIZUNGUMZIAJE YANGA?

“Yanga ni timu kubwa ambayo ina wachezaji wengi wazoefu lakini

binafsi  nilikuwa na ndoto ya kucheza Yanga tangu nilipokuwa mdogo kwa sababu nilikuwa na malengo nayo. “Cannavaro amekuwa chachu kubwa ya mimi kukubali kujiunga na Yanga kwa sababu alikuwa ananivutia sana tangu nilipokuwa mdogo, nikawa nafanya juhudi ili niweze kufi ka alipofi ka yeye. “Naamini kwamba mimi na wachezaji wenzangu tutafanya kazi kubwa msimu ujao kuhakikisha malengo yanafi kiwa kwa sababu kucheza hapa kwangu ni kitu kikubwa na ni heshima kwangu.

NASIKIA UNATAKA JEZI NAMBA 13, ILE KAMUSOKO?

“Yanga wamenipa jezi namba sita kutokana na ile niliyokuwa naipenda kuwa na mtu, sikuwa na jinsi kwa sababu naamini hata hii haiwezi kuniharibia kitu kwenye malengo yangu. “Binafsi napenda kuvaa jezi namba 13 (inavaliwa na Thabani Kamusoko), hiyo jezi nimekuwa nikiipenda tangu zamani kwa sababu  kuna shabiki wangu mmoja wakati najiunga na Taifa Jang’ombe aliwahi kuniambia kwamba huwa anapenda anione nikiitumia jezi hiyo, kwa kuwa namkubali nikaona niitumie na nimekuwa nikiipenda sana.

SIMBA INAMSAJILI OKWI, HII UNAIONAJE?

“Unajua Okwi ni mchezaji mzuri na kweli anasumbua sana lakini kama nitakuwa napata nafasi ya kucheza, nitajitahidi nimdhibiti asilete madhara kwetu. “Naamini ninao uwezo wa kummiliki hasiinyanyase Yanga kama alivyokuwa akifanya awali, huu ni mwisho wa Okwi kutamba kwa sababu najiamini sana. “Naiweza kazi ya kumdhibiti, nitampoteza na watu hawatamuona katika kiwango chake.”

Leave A Reply