The House of Favourite Newspapers

Ukweli Uongozi wa Manji Yanga Ulikuwa wa Mafanikio

0

MWANACHAMA wa Yanga, Yusuf Manji amekuwa ndani ya klabu hiyo kwa takribani miaka 13 akiwa katika sehemu mbalimbali. Kama mwanachama wa kawaida, lakini aliingia kama mfadhili na msuluhishi wa mgogoro kati ya Yanga

Kampuni na Yanga Asili, pembeni kukiwa na Kundi la Yanga Bomba. Baadaye akageuka kuwa mfadhili tu wa kufanya mambo yaende kwa mpangilio sahihi lakini mwisho akaamua kugombea na kuwa mwenyekiti. Manji aligombea uenyekiti mwaka 2012 baada ya Simba kuiangushia Yanga kipigo cha mabao 5-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa Mei 5, 2012 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wakati akitangaza kugombea uenyekiti, Manji alisema ameamua kurejesha umoja baada ya kipigo hicho ambacho aliamini kama klabu itaendelea kuwa katika hali ya taharuki, basi kuna hofu ya mambo kuvurugika kabisa. Kwa miaka minne aliyokuwa madarakani, Yanga ikabeba ubingwa wa Bara mara tatu, mara moja ikibeba Azam FC na huo ukawa mwisho wa Simba kubeba ubingwa hadi sasa.

Miaka yote minne, Yanga ikashiriki michuano ya kimataifa. Mwaka wa mwisho, Yanga ikabeba ubingwa wa Bara tena na Simba angalau imeamka na kubeba ubingwa wa Kombe la FA ikiwa imeonyesha matumaini ya kuamka upya. Wakati wa uongozi wa Manji, hakuna ubishi kwamba umekuwa wa mafanikio makubwa huenda kuliko kiongozi mwingine yeyote. Kumbuka miaka mitano, ubingwa mara nne na ku? ka robo fainali ya Kombe la Shirikisho.

Ndani ya uongozi wake pia kulikuwa na milima na mabonde, kwani walikuwepo ambao walikuwa wakimpinga wakiwa na hoja zao.

Hakuna kiongozi anayekubalika au anayeweza kuongoza bila ya kupingwa hata kidogo, hii haijawahi kutokea kokote duniani. Waliokuwa wakimpinga Manji, wengi walionyesha alikosea sana, walionyesha Yanga haikufanya lolote kwa maana ya kufanya vizuri. Wengine walidai aliwazuia kushiriki au kufanya mambo ya maendeleo katika klabu. Kulikuwa na kundi dogo la wanachama na mashabiki lililokuwa likilalamika kwamba halina nafasi.

Binafsi wako waliokuwa wana hoja, mfano wale ambao walipinga Yanga kufanya mambo ya mpito pekee, usajili mkubwa, kambi za nje ya nchi zilizojaa mbwembwe na hakukuwa na uwekezaji sahihi. Mfano angalau ujenzi w a uwanja wa mazoezi na hili nilili zungumza sana. Huenda Manji alitaka kuona Yanga inapata lile eneo ililoomba Jangwani ili kutimiza ndoto ya kujenga uwanja.

Hivyo hakuona sababu ya kuanza na uwanja wa mazoezi. Kuna ule msemo wa Kiswahili; “Baniani Mbaya, Kiatu Chake Dawa.” Ukweli ni kwamba Manji alifanya vizuri katika uongozi wake Yanga hata kama alikuwa na upungufu wake hadi alipo? kia kujiuzulu. Wote tunajua Manji aliifanya Yanga kuwa kubwa na ku? kia kuonekana si saizi ya timu nyingine. Kuna wakati alikopesha, kuna wakati alitoa msaada na wakati mwingine alibuni mipango kadhaa ya kuingiza fedha kwa klabu ingawa haikuwa endelevu.

Ukiangalia wenyeviti wengi waliopita, ni vigumu kuwalinganisha kimaendeleo na alichofanya. Bado ilionekana hana msaada kwa baadhi ya watu ambao walitaka aondoke huku wakisisitiza wako watu wengi wanataka kuiongoza Yanga lakini hawapati nafasi kwa kuwa Manji yupo. Kwa sasa wote tunajua kwamba hali ya Yanga kifedha si nzuri hasa baada Manji kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti. Usajili umekuwa ni wa kusuasua licha ya kwamba viongozi wanatembeza propaganda kuwa mambo ni sa? . Wana haki ya kufanya hivyo ili kujenga morali, lakini uhalisia hau? chiki na hapo ndiyo ninashangazwa.

Kwamba wale waliosema Manji aliwanyima nafasi vipi hawaji, mbona hatuwaoni? Walikuwa ni watu wa maneno tu? Walitaka kujisi? a tu? Walitaka kuonekana wanapambana na Manji ili watu wawaone nao ni wakubwa sana? Yanga inateseka, inahitaji fedha wakati huu kwa kuwa haikuwa na imewekeza katika vitu sahihi vingi, ilikuwa vya mpito na Manji angesaidia kwa mapenzi yake. Sasa hayupo, nyie mliotaka kuingia wakati ule, bilionea ambaye ilielezwa angejitokeza kuwekeza baada ya Manji kusema anataka kuikodisha Yanga yu wapi? Kama hamjitokezi sasa kuisaidia Yanga, itaonyesha kiasi gani watu wengi wa mpira ni wana? ki na mnapenda hadithi nyingi bila ya uhalisia. Mnapenda kuonekana lakini hamna nia njema! Yanga ni timu ya wananchi, yes! Sasa hao wananchi wako wapi, vipi sasa wasionyeshe ukubwa wa Yanga na kwamba haiwezi “kufa njaa.” Huu ndiyo wakati wa kuonyesha mapenzi yenu na kuthibitisha mliyoyasema katika kipindi Manji yupo na kwamba mnaweza sasa. Niwafundishe na wengine, hata kama Manji ana mabaya yake leo ameondoka, Simba wanasema wamepumua. Basi Yanga mjifunze kushukuru kwa kuwa wakati wake mliona hana lolote, angalieni leo, mna swali jingine?

Leave A Reply