The House of Favourite Newspapers

Yanga Kuingia Mafichoni Julai 2

0

KIKOSI cha Yanga hivi karibuni kinatarajia kuingia kambini kuanza kujiandaa kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ambapo kwa sasa kinachokwamisha kuanza kwa kambi hiyo ni ko­cha wao mkuu, George Lwan­damina raia wa Zambia am­baye bado hajarejea nchini.

Lwandamina aliyeipa ubingwa wa ligi Yanga msimu uliopita bado hajarejea nchini kutokana na kuwepo nchini kwao akimalizia mapumziko yake baada ya kumal­izika kwa ligi.

Akizungumza kupitia Kipindi cha Spoti Hausi ki­nachorushwa na GlobalTv Online, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Godlisten Anderson ‘Chicharito’ amesema kuwa kikosi hicho kimepanga kuanza kambi yake kuan­zia Julai 2 au 3, mwaka huu ambapo kambi hiyo itategemea na mawazo ya kocha huyo.

“Kinachotusubirisha kuan­za kambi yetu ni kocha Lwandamina ambaye bado hajarejea nchini kutoka kwao Zambia alipoenda kwa ajili ya mapumziko tan­gu ligi ilipomalizika, lakini tunategemea hivi karibuni atarejea na tutaanza kambi yetu.

“Kambi rasmi inaweza kuwa Julai 2 au 3, ila hatu­jajua ni wapi ambapo tu­taenda kuweka kambi hiyo mpaka kocha aje na kusema wapi twende japo kuna maeneo sita ambapo pamependekezwa kwenda kuweka kambi,” alisema.

Leave A Reply