The House of Favourite Newspapers

EBITOKE: Msiba wa Mfanyakazi Mwenzetu Umetushtua Sana

0
Ebitoke akihojiwa na Global TV Online.

 

KUFUATIA kifo cha Seth Katende ‘Bikira wa Kisukuma’, aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha Efm, kipindi cha Ubaoni, ambaye mwili wake umeagwa katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam na kuzikwa katika Makaburi ya Kinondoni leo Julai 12, 2017, msanii wa komedi, Ebitoke ameeleza majonzi aliyoyapata kufuatia msiba huo.

 

“Kwa kweli ni majonzi makubwa nimeyapa kutokana na msiba huu, kwa sababu alikuwa mfanyakazi mwenzetu pale TV E. Msiba umetushtua sana, ni majonzi makubwa kwa wanafamilia. Napenda kuwapa pole wote walioguswa na msiba huu,” alisema Ebitoke.

 

Bikira wa Kisukuma, alifariki juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwa mujibu wa baadhi ya wafanyakazi wenzake ambao hawakutaka kutajwa majina yao kwa vile siyo wasemaji, walisema marehemu alianza kuugua kiasi cha mwezi mmoja uliopita na msiba uko nyumbani kwa baba yake mzazi huko Changanyikeni.

 

Marehemu ambaye alikuwa akitangaza kipindi cha Ubaoni, kinachorushwa na redio hiyo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, saa kumi jioni, alikuwa pia ni bloga maarufu katika mitandao ya kijamii.

MSIKIE EBITOKE AKIELEZA MAJONZI YAKE

Leave A Reply