The House of Favourite Newspapers

Snura, Darassa hapatoshi Chato Jumamosi hii

0
Darassa.

HATOKI mtu! Unaweza sema hivyo kwa maana nyingine pale wakali wasioshikika kunako gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Mamaa Majanga’ na Sharif Thabeet ‘Darassa’  Jumamosi hii (Agosti 5) wanatarajiwa kutikisa kwa shoo ya kishindo katika uzinduzi wa hoteli ba’kubwa ya JS Motel iliyopo Chato mjini mkoani Geita.

 

Akizungumza na Risasi Vibes, Darassa anayebamba na Ngoma ya Hasara Roho pamoja na ngoma ya taifa ya Muziki alisema kuwa, kwa mara nyingine anarudi Chato lakini safari hii anarudi kuonesha burudani ya kishindo zaidi kwa kuwa itawahusisha wateja na waalikwa wote watakaofika katika uzinduzi wa JS Motel. “Huwa sikosei linapotokea suala la mualiko kama hili la uzinduzi.

 

Nashukuru kuwa miongoni mwa watakaozindua JS Motel ndani ya Chato Mjini kwa mara ya kwanza na ninachoahidi kufanya ni makamuzi ya live jukwaani nikipiga nyimbo zangu zote ikiwemo Too Much, Sikati Tamaa, Weka Ngoma pamoja na ngoma yetu hii ya taifa ya Muziki,” alisema Darassa.

Snura.

 

SNURA

Kwa upande wa Snura ama Mamaa Majanga kama wengi wanavyomuita alisema, siku hiyo ya uzinduzi atafanya tukio ambalo si la nchi hii kutokana na alivyojiandaa pamoja na madansa wake. “Mashabiki wote wanaifahamu shughuli yangu nikiwa katikati ya jukwaa.

 

Tena hii imekuja mahala pake kwani nitawazindulia ngoma yangu mpya hukohuko kwenye uzinduzi wa JS Motel, asikwambie mtu yaani nitakinukisha mwanzo mwisho, kuanzia Chura, Najibadua, Shindu, Ushaharibu, Majanga na nyingine kibao. Siku hiyo sitawaimbia tu, nitawapa staili mpya ya kucheza nyimbo hizo,” alisema Snura.

STORI: RISASI VIBES

                                                                                          ====

Wakili Apinga Ushahidi wa Mkemia Mkuu Kuhusu Mkojo wa Wema

Leave A Reply