UHAKIKI WA RIWAYA: TAKADINI (Sehemu ya Pili)
UJUMBE
Mafunzo yanayopatikana katika riwaya ya TAKADINI ni:
- Walemavu wana haki ya kuishi kama watu wengine. Asitokee mtu yeyote wa kuyakatisha maisha ya mlemavu kwa sababu ya imani potofu.
- Mlemavu anaweza akafanya mambo yenye faida kwa jamii, pengine kuzidi wasio walemavu. Takadini aliisaidia jamii yake, kijana huyu alikuwa muimbaji mzuri pia alikuwa mganga aliyetibu wagonjwa mbalimbali.
- Ujasiri unahitajika katika kupambana na imani potofu. Sekai anatumia ujasiri kupambana na mila potofu zilizotaka mwanaye auawe. Katika wakati huu mgumu, anaibuka mshindi aliyezipiku na kuziangusha mila hizo… SOMA ZAIDI