The House of Favourite Newspapers

UVCCM: Wahandisi Zanzibar Jengeni Barabara Bora

0
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umekemea baadhi ya wahandisi wasiowajibika ipasavyo kwa kujenga barabara chini ya kiwango ilihali serikali imewalipa fedha zao kadri ya makubaliano.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (kushoto) akiongea na Mhandisi Amin Khalid Abdallah (kulia) alipokwenda kukagua ujenzi wa barabara wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.  
Shaka akipokewa katika Hospitali ya Chakechake Dkt. Ali Habib Ali alipowasili hospitalini hapo kuangalia wagonjwa na kuwafariji.
 
…Akimpatia baadhi ya vifaa-tiba Bi Salha Issa Nassor alipotembelea wodi ya kinamama waliojifungua katika Hospitali ya Wilaya ya Chakechake.
 
…Akiwasili katika ukumbi wa mkutano Tawi la CCM Wawi kuzungumza na Vijana wa CCM.
 
 
Vijana wakifuatilia mkutano huo.
 
Shaka akizungumza na Vijana wa CCM. 
…Akizungumza na maofisa wadhamini wa mabaraza ya mji na madiwani.
Maafisa wadhamini wa mabaraza ya mji na madiwani wakimsikiliza Shaka.


UVCCM imesema kuwa serikali inapaswa kuwachukulia hatua za kisheria wahandisi hao ikiwemo kuwanyima tenda sambamba na kuwafikisha mahakani kwani wanaisababishia hasara kubwa serikali kwa kufanya marekebisho ya barabara mara kwa mara.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka leo alipokuwa akikagua ujenzi wa barabara ya OleVitongoji na Mfukiwa-Kengei wakati wa ziara ya kikazi ya ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Unguja.

Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 35 inatarajiwa kukamilika katika hatua za awali mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu huku ukamilisho wote ukitarajwai kufika ukomo Desemba mwaka kesho.

Shaka amepongeza namna barabara hiyo inavyojengwa kwa viwango ambayo itakuwa na uwezo wa kudumu kwa muda mrefu pasina kufanyiwa marekebisho ya mara kwa mara kama ambavyo baadhi ya barabara zimekuwa zikiharibika na kufanyiwa marekebisho jambo ambalo linaiingizia serikali hasara.

Hadi kufika hatua ya ukamilisho barabara hiyo itagharimu Dola za Marekani milioni 11 ambazo ni sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 24.4

Barabara hiyo inajengwa na Wizara ya Ujenzi na Utunzaji wa Barabara Zanzibar upande wa Pemba kupitia ufadhili wa mfuko wa nchi zinazotoa mafuta kwa wingi duniani (OPEC).

Naye Meneja Mradi wa barabara hiyo Mhandisi Amin Halid Abdallah amempongeza Shaka kwa kuzuru eneo hilo kujionea hali ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM huku akiahidi kusimamia ujenzi huo kwa weledi na hatimaye kuwa na barabara imara.

Na Mathias Canal, Kusini Pemba

Leave A Reply