The House of Favourite Newspapers

Yanga Yapata Mrithi Wa Ally Yanga

0

 

Shabiki mpya wa Yanga, Mack Yanga.

 

HIVI karibuni Yanga ilimpoteza shabiki wake maarufu, Ally Mohamed ‘Ally Yanga’ ambaye alifariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea Mpwapwa, Dodoma.

Ally Yanga alijulikana kwa staili yake ya kujipaka masizi usoni, kuweka kitambi cha bandia ambapo alikuwa akichukuliwa pia kwenda kuishangilia Taifa Stars ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo, hivi karibuni ameibuka shabiki mwingine wa timu hiyo ambaye aina yake ya ushangiliaji ni kama ile ya Ally Yanga, huyu wa sasa anaitwa Mack Yanga.

Akionyesha manjonjo yake.

Championi Ijumaa ilizungumza na shabiki huyo aliyekuwepo uwanjani wakati Yanga ikicheza mechi ya kirafiki na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Azam Complex, wiki iliyopita.

“Nilikuwa shabiki mkubwa sana wa Ally Yanga na baada ya kifo chake niliumia sana, kwa hiyo ili kumuenzi basi bora niige aina yake ya ushangiliaji wake,” alisema.

 

Leave A Reply