MKUTANO WA 37 WA SADC WAMALIZIKA MJINI PRETORIA
Makamau wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini moja ya makubaliano katika mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano huo mjini Pretoria.
Dkt. Stergomena Tax akila kiapo mara baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa SADC .
Makamau wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini moja ya makubaliano katika mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano huo mjini Pretoria.
Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kuteuliwa na kula kiapo kuwa Katibu Mtendaji wa SADC .
Amesema Tanzania imeshakuwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo mara tatu, kwa nyakati tofauti ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni kipindi cha 2006/2007 na mara ya pili ilikuwa ni 2012/2013 na mara ya tatu katika kipindi cha Agosti 2016 hadi Agosti 2017 chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo alikabidhiwa kijiti cha uongozi huo kutoka kwa Jamhuri ya Msumbiji wakati wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika Falme ya Swaziland tarehe 30 Agosti, 2016.
Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana wakati wa Uenyekiti wa Tanzania katika Asasi hiyo ni kusimamia uchaguzi wa Bungenchini Seychelles ambao ulifanyika mwezi Septemba, 2016.
Aidha katika kipindi cha Uongozi wa Tanzania ulisaidia kurejesha hali ya amani na utulivu nchini Lesotho ambayo kwa muda mrefu tangu 2014 imekuwa kwenye mgogoro wa kisiasa pamoja na kushughulikia matatizo ya Uchaguzi nchini DR Congo.
Mkutano wa 37 wa SADC pia umemuongezea muda mwingine Mtanzania Dkt. Stergomena Taxi kuendelea na wadhifa aliokuwa nao wa Katibu Mtendaji wa SADC kwa kipindi cha miaka minne mingine ambapo atatumikia nafasi hiyo hadi mwaka 2021.
Dkt. Tax amethibitishwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliomaliza leo na kuapishwa rasmi kushika nafasi hiyo.
Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali (SADC) umehitimishwa kwa kutolewa Tamko (Communique) kuelezea yaliyojiri katika Kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali ikiwa ni pamoja na mkutano wa 38 kufanyika nchini Namibia
Imetolewa na ;
Ofisi ya Makamu wa Rais
Pretoria, Afrika Kusini
20 Agosti, 2017.