The House of Favourite Newspapers

Kocha: Yanga Tayari Wamekwisha

0

 

Wachezaji wa timu ya Simba.

KOCHA Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja ameibuka na kufunguka kuwa kwenye mchezo wa leo mbele ya Yanga hawana cha kupoteza huku wakiingia uwanjani wakiwa na lengo moja pekee la kushinda.

Mayanja aliyewahi kuinoa Kagera Sugar ya Kagera leo Jumatano atashirikiana na bosi wake, Joseph Omog raia wa Cameroon kusaka taji la Ngao ya Jamii kwa kuivaa Yanga, kwenye mechi itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mayanja amesema kuwa kutokana na aina ya kikosi walichonacho ni imani yake kuwa wana kila sababu ya kuibuka na ushindi mbele ya Yanga na kuanza vizuri msimu wa 2017/18.

Wakiendelea na mazoezi.

“Tunawaza kuanza vizuri msimu kwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii, ambalo kama tutalipata naamini litakuwa sababu kubwa kwetu kuwa na msimu mzuri wa ligi kwa sababu wanasema nyota njema huanza kuonekana asubuhi.

“Naamini kabisa sisi tutashinda mechi hii kwa sababu tumepata muda mzuri wa kujiandaa na kupanga mipango yetu vizuri kabisa, yaani kikosi tulichonacho kinanipa imani kabisa ya kuona tayari tumeshawamaliza Yanga ila kilichobakia ni kwenda kukithibitisha uwanjani tu,” alisema Mayanja.

Stori: Said Ally, Championi Jumatano

Leave A Reply