The House of Favourite Newspapers

DERBY DAY EPL LEO HAPA ARSENAL PALE CHELSEA

0

Kwenye ligi kuu ya Uingereza leo ni usiku wa Derby ambapo watakutana miamba miwili ya soka kutoka katika jiji la London ambao ni klabu ya Arsenal washika mitutu dhidi ya matajiri wa jiji hilo klabu ya Chelsea.

Kipute hichi kikali kitapigwa pale katika dimba la Emirates baada ya mchezo wa kwanza kupigwa katika dimba la Stamford Bridge kumalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili huku ikisubiriwa usiku wa leo nani ataibuka mbabe.

Mchezo huu ni muhimu kwa vilabu vyote viwili kwani klabu ya Arsenal ambao ni vinara mpaka sasa wa ligi kuu ya Uingereza wao watahitaji kushinda mchezo huu kwa kiwango kikubwa ili kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa huo msimu huu.

Chelsea wao pia mchezo utakua muhimu sana kwao kwani wakifanikiwa kushinda mchezo huu watakua na matumaini ya kucheza michuano ya ulaya mwakani,Ambapo kama watakosa ligi ya mabingwa basi watapata Uefa Europa league au Uefa Conference League.

Suka mkeka wako kwenye michezo mikali itakayopigwa leo kwenye michuano mbalimbali barani ulaya na duniani kote. Machaguo zaidi za 1000 yapo huku lakini vile vile Turbo Cash pia ipo. Unasubiri nini sasa? Ingia meridianbet na ubashiri sasa.`

Timu hizi zinakutana ambapo Arsenal atakua na kumbukumbu ya kusimamishwa na Chelsea wakiwa na fomu nzuri kabisa na kulazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili, Hivo mchezo wa leo ndio utaamua ni nani mbabe wa mwenzake katika msimu huu wa 2023/2024.

Leave A Reply