The House of Favourite Newspapers

Idris Abanwa Kumchunia Wema

0

 

Idris Sultani akiwa na Wema Sepetu.

 

MCHEKESHAJI mwenye jina kubwa Bongo, Idris Sultani hivi karibuni amebanwa juu ya madai ya kumchunia mrembo Wema Sepetu kutokana na kutohudhuria kwenye uzinduzi wa brand yake ya viatu iitwayo Fareman na kufunguka kuwa kwa upande wake amekwisha msamehe mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006.

Idris alisema kwamba ni kweli Wema hakuhudhulia kwenye uzinduzi wake huo bila kumpa taarifa yoyote lakini kwake hilo si tatizo na kwamba amekwishamsamehe bila hata kuzungumza naye.

“Sina tatizo na Wema kabisa, ni mshikaji wangu wa karibu kwa kutohudhuria kwenye hafla yangu maana ninafahamu alikuwa na mambo yake mengine na hakuna ukweli kwamba nimemchunia,” alisema Idris.

Stori: Boniphace Ngumije

Baada ya Bongo Muvi Kufa, Yafufuka Kupitia BARAZANI

Leave A Reply