The House of Favourite Newspapers

Lipstick Za Wema Zadaiwa Kupigwa ‘Stop’!

0
Staa mwenye jina kubwa ndani na nje ya Bongo, Wema Isaac Sepetu.

KAMA ilivyo ada ya ubuyu kutoka visiwani Zanzibar, huwa haumuachi mtu salama kutokana na namna unavyoandaliwa! Ndivyo ulivyo ubuyu wa wa motomoto uliotufikia kunako meza ya kujilamba kuwa, staa mwenye jina kubwa ndani na nje ya Bongo, Wema Isaac Sepetu anadaiwa kupata pigo baada ya mzigo wake mkubwa wa zile lipstick zake za Kiss kuzuiwa kuingizwa Bongo na taasisi moja serikalini.


UNAKUMBUKA ZILE LIPSTICK ZA WEMA?
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu wa ubuyu, badaa ya lipstick alizozitoa mwanzoni kugombewa kama njugu na wasambazaji mbalimbali wa urembo wa jumla na rejareja Bongo, inasemekana kuwa, mlimbwende huyo alinogewa na mambo ya fedha hivyo akaagiza mzigo mwingine kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuendeleza biashara hiyo.
Hata hivyo, chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa, kutokana na namna bidhaa hiyo ilivyokubalika na kupendwa na wanawake wa rika mbalimbali, Wema alipata shauku kubwa na kuagiza mzigo mkubwa zaidi.

 

“Unajua ule mzigo wa kwanza wa Wema, watu waliupenda sana na kuugombea sana hivyo aliamua kuagiza mwingine tena kwa ajili ya kuendelea na biashara yake kwa kuwa mzigo haukukaa sana,” kilinyetisha chanzo hicho.
Mtoa habari huyo alizidi kutiririka kuwa, baada ya Wema, kuagiza mzigo huo, ulifika Bongo, lakini kisheria lazima upitie kwenye taasisi moja serikalini ili kuthibitisha kama zina ubora.

 

ZADAIWA KUPIGWA ‘STOP’
Ilidaiwa kuwa, katika hatua hiyo ndipo zilipogundulika kuwa hazina kiwango au ubora kwa afya ya binadamu hivyo kupigwa ‘stop’ kusambazwa Bongo.
“Wale jamaa walisema hauna kiwango sahihi kwa ajili ya kuwauzia watu hivyo ukazuiliwa na hakuweza tena kuusambaza na kuamua kukata tamaa,” kilizidi kufunguka chanzo hicho.

 

KADINDA ASAKWA
Baada ya Ijumaa Wikienda kumwagiwa ubuyu huo lilianza kusaka njia za kuthibitisha madai hayo ambapo lilianzia kwa mmoja wa mameneja wa Wema, Martin Kadinda.

Kadinda alipobanwa juu ya ubuyu huo alisema kuwa, anachokijua ni kwamba Wema alitoa zile lipstick za mwanzo hivyo kama kuna zilizopigwa stop, zitakuwa ni za mtu mwingine ambaye alitaka kuziingiza nchini kwa kutumia jina la bosi wake huyo.

 

“Ninachojua ni kwamba Wema alitoa zile za kwanza tu, kama kuna za pili, sina uhakika maana kama zilitoka mimi ningejua.
“Inawezekana kabisa katika mazingira tuliyo nayo, kuna mtu anaweza akawa anatumia jina lake (Wema), lakini siyo yeye kabisa,” alisema Kadinda.
Jitihada za kuzungumza na Wema hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kupigwa mara kadhaa lakini haikupokelewa. Hata alipotumiwa ujumbe mfupi na chatting kwa njia ya WhatsApp hakujibu.

 

NENO LA MHARIRI
Kazi ya Ubuyu Ulionyooka ni kuupokea ubuyu kutoka kwa chanzo kisha kuutafutia ladha maridhawa na kuufikisha kwako ili uumung’unye kwa raha zako na hicho ndicho tulichokifanya.

Baada ya Bongo Muvi Kufa, Yafufuka Kupitia BARAZANI

Leave A Reply