The House of Favourite Newspapers

Julio Anadai Ndiyo Kwanza Imeanza

0
Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.

KOCHA Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema baada ya kuiongoza timu yake ya Dodoma FC kushinda bao 1-0 dhidi ya Pamba SC katika Ligi Daraja la Kwanza, ndiyo kwanza kazi imeanza na atahakikisha anashinda kila mchezo ulio mbele yake.

Ikicheza kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma wikiendi iliyopita, Dodoma FC ilishinda bao 1-0 dhidi ya Pamba ambayo ilitamba katika soka la Tanzania katika miaka ya nyuma.

Akizungumza na Championi Jumatano baada ya mchezo dhidi ya Pamba, Julio alisema timu yake imejipanga kupanda daraja hadi Ligi Kuu Bara msimu ujao na watapambana kupata nafasi hiyo.

“Dodoma FC tumejipanga kupanda daraja kwani tulifanya maandalizi mapema hivyo mashabiki wetu watuunge mkono kwani kwa ushindi huu tuliopata dhidi ya Pamba ni kwamba kazi ndiyo imeanza,” alisema Julio.

“Ligi daraja la kwanza ni ligi ngumu lakini tumejipanga kufanya vizuri katika michezo yetu.”

Msimu wa mwaka 2016/17, Julio ambaye wakati huo alikuwa akiifundisha Mwadui FC alitangaza kuachana na soka kutokana na madai kuwa waamuzi wamekuwa wakichezesha bila kufuata kanuni 17.

Young Killer Aliamsha Dude! Adai Dogo Janja na Young Dee Hawamuwezi

Leave A Reply