The House of Favourite Newspapers

Chuz Adaiwa Kuvuruga Ndoa Ya Msanii Wa Bongo Fleva

0
Staa wa filamu za Kibongo, Tuesday Kihangala ‘Chuz’.

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva aliyetamba na Ngoma ya Binti Mlokole, Jimmy Gulam ‘Father G’ ameibuka na kumlalamikia staa wa filamu za Kibongo, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ kumvurugia ndoa yake baada ya kudai kwamba amemfumania na msanii wake wakati wakiwa kambini.

 

Akizungumza kwa huzuni, Father G alisema habari za kwamba amefumaniwa na msanii Noela Mkwizu ‘Kanjo’ ambaye walikuwa kambini huko Lushoto, Tanga wakicheza tamthiliya ya Chuz ya Closed Chapter zimesababisha vurugu kubwa  kwenye ndoa yake na mkewe amerudi kwa wazazi wake.

 

“Chuz amevuruga ndoa yangu baada ya kunifukuza kambini na kudai amenifumania na huyo Kanjo wakati ni mwanamke wake sasa ningewezaje kuwa naye kimapenzi, siyo kweli kabisa habari hizo zimetengenezwa kwani siku ya tukio msichana huyo alikuja kwenye chumba changu kuangalia TV lakini ghafla alipokutwa wakasema wametufumania, kiukweli Chuz amenichafulia sana jina langu na familia yangu kwa ujumla,” alisema Fadher G.

Leave A Reply