The House of Favourite Newspapers

Kilio Chetu Kwa Waamuzi Bado Kinaendelea

0

KUNA wakati tunasema kuna aibu za kujitakia tu hilo linatokana na kama unafanya jambo la hovyo wakati ulikuwa na uwezo wa kuliepuka. Ni watu wengi tu au taasisi nyingi hapa nchini zinafanya makosa ya kujitakia na kupata aibu ambazo wangeweza kuiepuka.

 

Jumamosi iliyopita nilikuwa mmoja ya watazamaji, nilienda kuangalia mechi ya kirafiki baina ya Taifa Stars dhidi ya timu ya taifa ya Malawi na nilichokiona huko kutoka kwa muamuzi, nina­muachia mwenyezi Mungu.

 

Sijui waamuzi wetu wanakum­bwa na pepo gani? Mara nyingi najiuliza hili swali lakini ninakosa jibu kabisa. Hawa ndugu zetu bado wanatupa shida sijui wa­taendelea hivi hadi lini? Maana tu­meshawachoka na kuharibu kwao lakini hawabadiliki miaka nenda miaka rudi.

 

Kwenye michezo ya ligi zetu hapa nyumbani kama Ligi Daraja la Kwanza au Ligi Kuu Tanzania Bara tumeshazoea huko kuharibu kwao lakini inapofika hadi kwenye michezo ya kimataifa hapo in­atupa shaka zaidi.

 

Ninasema hivyo kwa kuwa in­atupa shaka sababu watu wame­kuwa wakisema eti waamuzi wetu wanafanya vizuri mno wakicheze­sha mechi za kimataifa na sasa Mungu alituonyesha uongo wao mbele yetu.

 

Tulipata aibu mbele ya Wama­lawi wale wachache waliokuwe­po uwanjani kisa mtu mmoja tu aliyesimama katikati kuhukumu mchezo ule na akashindwa kuifan­ya ile kazi ipasavyo na hilo ndiyo tatizo.

 

Sijui tufanye nini ili waamuzi wetu waweze kutuelewa sijui ha­wajui kama wanatukera kwelikweli na tumechoshwa na huko kuvu­runda kwao kila siku.

 

Hapo juu nilianza kwa kusema kuwa ni aibu ya kujitakia, ni kweli nilichokiona ni aibu ya kujitakia kwa wakuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa sababu wa­likuwa na uwezo mkubwa wa ku­leta mwamuzi kutoka nje ya nchi kuchezesha mchezo huo, hata kama inegkuwa kutoka nchi jirani tunazopakana nazo.

 

Basi kama ingeshindikana kabisa wangechukua waamuzi kutoka Zanzibar na siyo waamuzi hawa wa huku Bara ambao wengi wao tunawajua maana kuvurunda kwao imekuwa ni sehemu ya mai­sha yao yaani hakuna jipya.

Kwa mfano kocha wa Malawi siku ile alitolewa kwenye benchi kwa kuililia haki yake na wote tu­liona lazima tuseme kweli na tu­muogope mwenyezi Mungu.

 

Mpira ulitolewa na mmoja ya wachezaji wa Taifa Stars, ilibidi iwe kona lakini muamuzi yule aka­wanyima kona Malawi ndipo kocha wao alipoanza kulalama kuililia haki yake na kwa kujisafisha ndu­gu yangu muamuzi akaamua kum­toa kwenye benchi na kumpeleka jukwaani kwa mashabiki.

 

Kwa ufupi mimi nimeshawa­choka hawa waamuzi wetu basi tu sina la kufanya lakini wanayoya­fanya kwenye soka letu ni madudu matupu ambayo hayawawezi ku­vumilika hata kidogo.

 

Mwisho kabisa naomba msalim­ieni Salum Mayanga na mwambie kazi njema ya kuendelea kujenga timu na sijui tutakuwa tunajenga timu hadi lini? Lakini ndiyo hivyo tuendelee kupambana na hali zetu.

 

Nadhani Mayanga atakuwa amejifunza kitu kwenye mchezo ule dhidi ya Malawi kama wana­vyosema Waswahili kuwa ‘Wali wa kushiba unaonekana kwenye sa­hani’.

Leave A Reply