The House of Favourite Newspapers

Jogging 200 Kukutana Dar Live Jumapili

0

MAGENGE 20 Jogging and Sports Club kwa kushirikiana na Dar Live wamejipanga kuvikutanisha vilabu vya jogging na gym zipatazo 200 ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini, Jumapili hii.

 

Kongamano hilo limepewa jina la Dar es Salaam Jogging and Aerobics huku kauli mbiu ikisema; “Hamasisha Familia Yako Kufanya Mazoezi Kwa Afya Bora.”

 

Akizungumza na Gazeti la Amani, Meneja wa Dar Live ambaye ni Mratibu wa Bonanza hilo, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, vilabu hivyo vitaanzia Uwanja wa Polisi Maturubani-Mbagala Kizuiani na kumalizia katika Ukumbi wa Dar Live.

 

“Jogging zimejipanga kuhamasisha familia kufanya mazoezi kwa ajili ya kujenga afya bora katika kila familia. Kutakuwa na vilabu gym 200 mbalimbali za Jiji la Dar pamoja na michezo tofautitofauti ikiwemo netball, kukimbiza kuku, kuvuta kamba na mingineyo, alisema ‘KP Mjomba.”

 

Baadhi ya vilabu vitakavyoshiriki ni Bagamoyo Jogging, Mapinga, Temeke, Temeka Family, Faita Jogging, Wakali. Tupo Jogging, Dovya Jogging, Teacher Gym, Jo’s, Viva Gym na nyinginezo.

STORI: MWANDISHI WETU | AMANI

Leave A Reply