The House of Favourite Newspapers

Rammy Afunguka Kubanjuka Na Nikole

0
Naomi Salakikya ‘Nikole’ akiwa na Rammy Galis (kulia).

MSANII wa filamu Bongo, Rammy Galis amefungukia nyepesi za kuwa anabanjuka na msanii mwenzake, Naomi Salakikya ‘Nikole’ kwa kusema hakuna kinachoendelea baina yao, ni uzushi tu wa watu.

 

Akipiga stori na Showbiz-Xtra, Rammy alisema maneno hayo yalianza kuibuka kutokana na ukaribu mkubwa waliokuwa nao kipindi wanazindua muvi ya Red Flag siku chache zilizopita, ambayo walishirikishwa na waandaaji kutoka Nigeria.

 

“Acha watu waongee wanavyojisikia, ukweli ni kwamba Nikole ni mtu wangu wa karibu, kama rafiki yangu, kama dada yangu si mambo ya mapenzi kama watu wanavyodhani, si unajua Wabongo kwa kujiongeza,”alisema Galis.

STORI: MAYASA MARIWATA | AMANI | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply