The House of Favourite Newspapers

Mshindi Wa Nyumba Aanika Ya Moyoni

0
Mshindi wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, George Majaba wa Dodoma akiongea na wana habari.

MSHINDI wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, George Majaba wa Dodoma, ambaye alipokewa kifalme Jumanne iliyopita wakati akiwasili kwa ajili ya kukabidhiwa mjengo wake wa kisasa, ameanika mambo yake ya moyoni mwake kuhusu Global Group, waendeshaji wa mchezo huo.

 

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Sinza Mori, Majaba, aliyeambatana na mke wake, Neema pamoja na familia yake ya watoto watatu, alisema alianza kununua magazeti ya Global Publishers tangu yakiuzwa kwa shilingi mia mia, zaidi ya miaka 17 iliyopita.

George Majaba akiwa na majirani zake wapya wa Bunju B kwenye nyumba yake mpya, hapo walikuwa wakimkaribisha.

“Mimi hapa ni nyumbani, nimeanza kununua magazeti haya tangu yanauzwa shilingi miamia, yana habari nzuri, yanafundisha na kuburudisha. Mimi ni mpenzi sana wa michezo, hata lilipokuja kuanzishwa gazeti la Championi, ndiyo kabisa nikawa kama nimelogwa, ili upate habari bora kabisa za michezo, ni mpaka usome hili gazeti.

 

“Kuna kitu kimoja ninataka kukisema, tena kwa uwazi kabisa, serikali inapaswa kuiangalia vizuri kampuni hii kwa sababu inawasaidia sana watu wa hali ya chini, ingepunguziwa au kuondolewa baadhi ya kodi ili itimize majukumu yake sawasawa.

 

“Kuna kampuni zinapewa misamaha ya kodi lakini zikiwa hazina faida kwa watanzania, lakini angalia kampuni hii, inatoa nyumba kwa mara ya pili sasa, hili siyo jambo dogo hata kidogo, ningeiomba serikali kwa kweli iwaangalie, mnafanya jambo kubwa sana, huwa ninasoma jinsi mnavyowasaidia watu wenye uhitaji, kwa kweli hii ni kampuni ya jamii.

Ndani ya nyumba kushoto, George Majaba, Afisa Masoko, Jimmy Haroub, Mkurugenzi Mtendaji, Eric Shigongo, mke wa Majaba, Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho na Mhariri Mwandamizi, Elvan Stambuli wakifurahia mandari ya nyumba.

“Nyinyi mnasema mnatoa kidogo mnachopata kwa wasomaji wenu, niwaambie kitu cha kweli, hiki siyo kitu kidogo, ni kitu kikubwa sana hiki, ambacho mtu siyo rahisi kupata. Mimi sikuwahi kuwa na ndoto za

kumiliki nyumba hapa Dar, kwa sababu ni jambo gumu sana mtu kujenga hapa, lakini ninashukuru kwamba na mimi leo hii nina nyumba hapa.

 

“Hii isingewezekana kama siyo nyinyi, ambao mlikaa na kufikiri juu ya hii kitu. Sisi tunanunua gazeti kwa shilingi mia tano ili tupate habari, lakini mkaona hii haitoshi, mkatuwekea na kuponi ambayo tunaipata bure, ili mtuzawadie, siyo kitu rahisi, ndiyo maana utaona japo kuna kampuni nyingi za magazeti, lakini hazifanyi kama nyinyi mnavyofanya, ninawashukuru sana kwa mara nyingine,” alisema.

 

Awali, Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo alisema moyo wake umefarijika baada ya mshindi huyo kuwa ni mtu sahihi mwenye uhitaji, kwani lengo lao siku zote ni kubadili maisha ya wasomaji wao.

Hii ni mara ya pili kwa Global Group kutoa zawadi ya nyumba kwa wasomaji wake, kwani mara ya kwanza ilifanya hivyo mwaka jana, kwa msomaji wake Nelly Mwangosi kushinda bahati nasibu hiyo na kujitwalia nyumba ya kisasa iliyojengwa maeneo ya Salasala, jijini Dar.

Leave A Reply