The House of Favourite Newspapers

Shamsha: Nimeridhika Sina Mimba Jamani

0
Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford.

STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa hana mimba kama wengi wanavyodhani bali amenenepa kwa kuwa ameridhika na maisha anayoishi.

 

Shamsa aliyasema hayo baada ya hivi karibuni habari kuzagaa kwamba ni mjamzito ambapo watu mbalimbali walionekana wakimpongeza baada ya kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Instagram inayomuonesha akiwa amenenepeana sana ambapo aliliambia Risasi Jumamosi kwamba hana ujauzito bali amenenepa tu.

 

“Nimenenepa tu sina hata ujauzito jamani, nimeridhika na maisha yangu ila naona watu wanazungumza sana mara nina mimba, siku nikiwa nayo nitaweka wazi tu jamani wala wasiwe na wasiwasi ila kwa sasa bado mpaka mwaka ujao Mungu akipenda,” alisema Shamsa.

STORI: GLADNESS MALLYA

Leave A Reply