The House of Favourite Newspapers

Ester, Aunt Ezekiel Wamaliza Bifu Lao

0
Aunt Ezekiel

BAADA ya mastaa wawili wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel na Ester Kiama kuwa kwenye bifu la muda mrefu ambalo hawakuwahi kuweka wazi chanzo chake, hatimaye wamemaliza tofauti zao.

Aunt Ezekiel na Ester Kiama (kulia) wakiwa pamoja.

Chanzo makini kililieleza Risasi Jumamosi kuwa mastaa hao kwa sasa ushosti wao umerudi kama zamani na wamemaliza bifu lao ambalo limedumu kwa muda mrefu tangu mwaka jana licha ya kwamba hawajawahi kusema chanzo ni nini ila habari zinadai kwamba ni maneno ya uchonganishi baina yao.

Ester Kiama

Alipoulizwa Ester alikiri kwamba ni kweli wamepatana, waliamua wao wenyewe kumaliza tofauti zao na siku nyingi tu urafiki umerudi kama kawa.

STORI: GLADNESS MALLY

 

@auntyezekiel ake

A post shared by Ester Kiama. (@esterkiama) on

Leave A Reply