The House of Favourite Newspapers

Omog:Tunachukua Pointi Tatu Mbeya City

0
Kocha wa Simba, Joseph Omog.

KOCHA wa Simba, Joseph Omog ametamba kukiandaa vizuri kikosi chake na kusema atahakikisha wanaifunga Mbeya City, kesho Jumapili na kuchukua pointi tatu za Ligi Kuu Bara.

 

Simba iliwasili Mbeya, jana tayari kwa mchezo huo wa kesho ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo huku ukitarajiwa kuwa na upinzani mkubwa.

 

Simba ndiyo inayoongoza ligi ikiwa na pointi 16 sawa na Yanga, Mtibwa Sugar na Azam FC lakini yenyewe ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

 

Msimu uliopita zilipokutana timu hizi kwenye uwanja huo, Simba ilishinda mabao 2-0 na katika mechi nyingine jijini Dar es Salaam, walitoka sare ya mabao 2-2.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Omog alisema; “Tumejiandaa kikamilifu kuelekea mechi hiyo ili tushinde na kuendelea kukaa kileleni licha ya upinzani tutakaokutana nao dhidi ya Mbeya City.

 

“Mbeya City ni moja kati ya timu yenye upinzani mkali, lakini tumejiandaa kwa umakini wa hali ya juu kuelekea kwenye mechi yetu dhidi yao, tunahitaji kushinda ili tubaki kileleni.

 

“Tunajua mchezo hautakuwa rahisi, Mbeya City ni timu nzuri hivyo tunajiandaa kuhakikisha tunafanikiwa kushinda, kikosi changu chote kipo vizuri,” alisema Omog.

Hapa tumekuanikia kurasa za mbele na za nyuma za magazeti yote ya Tanzania leo, Novemba 4, 2017. Ni yale ya Hardnews, Udaku na Michezo.

Stori: Khadija Mngwai | Championi Jumamosi

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

Leave A Reply