The House of Favourite Newspapers

Hatimaye Sanchez Avaa Jezi ya Man U kwa Mara ya Kwanza

MSHAMBULIAJI Alexis Sanchez raia wa Chile ameonekana akiwa katika uzi wa Manchester United namba 7 saa chache baada ya usajili wake kukamilika akitokea Arsenal.
SNyota huyo anatarajia kutangazwa rasmi ndani ya saa 24 rasmi akiwa mchezaji wa Manchester United. Katika picha ya uficho, Sanchez anaonekana akipiga picha hiyo akiwa ndani ya Uwanja wa Manchester United, Old Trafford ambapo inaelezwa amepelekwa OT kwa ajili ya kupiga picha maalum.
Raia huyo wa Chile kutoka Arsenal, anatarajia kuwa akilipwa pauni 600,000 kwa wiki zitakazomfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi ndani ya klabu hiyo. Mgawanyo wa fedha hizo uko mshahara pauni 350,000, haki za picha pauni 100,000 na bonas itakuwa pauni 144,000.

Comments are closed.