The House of Favourite Newspapers

Simba Mkiwa Na Haraka Na Lechantre, Mtajivuruga Wenyewe…

Kocha Pierre Lechantre akiongea.

 

HATIMAYE lile suala la subira ya kocha mpya wa Simba sasa lime­pata jibu kwa kuwa Kocha Pierre Lechantre ameanza kazi yake rasmi juzi kukinoa kikosi chake baada ya kuka­milisha kila kitu.

 

Lechantre raia wa Ufaransa, anasaidiwa na makocha wen­gine wawili ambao ni Masoud Djuma raia wa Burundi pamo­ja na Mohamed Habibi kutoka Tunisia ambaye amejiunga na Simba akiwa pamoja na Lechantre.

 

Kocha huyo Mfaran­sa alitaka kujiunga na Simba akiwa na mtu kama Habibi ambaye anajua nini ampe cha kufanya na ame­kuwa akifanya naye kazi katika sehemu mbalimbali. Uongozi wa Simba umeku­bali ombi lake lakini umebaki na Djuma ambaye ameonye­sha ni kocha anayeiweza kazi yake.

Akifanya yake.

Kuanza kazi kwa Lechan­tre na wasaizidi wake, maana yake Simba imekamilisha jam­bo moja inawezekana kabisa ni wakati mwafaka kuhamia katika jambo jingine kwa ajili ya muendelezo wa sahihi ki­nachotakiwa.

 

Unapokuwa na jambo fu­lani linalokusumbua, kawaida ukifanikiwa lazima kuna jin­gine linakuja mbele. Simba hawawezi kuwa na shida ya kocha pekee. Badala yake kuna mengine ya maendeleo yanafuatia na lazima wayat­ekeleze.

 

Kwa kuwa kama uongozi wametekeleza hilo moja, ku­nakuwa na majukumu men­gine wanaendelea nayo kama kumuunga kocha huyo mkono katika masuala kadhaa kama atataka vifaa husika, uwanja wa mazoezi, kambi nzuri na kadhalika.

 

Simba wasitegemee kuona matunda bora kutoka kwa Lechantre na wasaidizi wake wakati wao hawatakuwa na ushirikiano na kocha huyo au kupuuzia mambo ambayo ata­waambia anahitaji kwa muda fulani ambao atawaeleza.

Kumekuwa na tabia, kocha anaingia kwa mbwembwe na viongozi watamuona kama lulu. Wakimzoea, basi ana­kuwa wa kawaida na mambo yanakwenda kama zamani.

 

Huo ni upande wa viongozi, kwa mashabiki wa Simba kwa kuwa wamekubali mabadiliko na walionekana wangependa kupata kocha mpya atakay­eendana na ukubwa wa Sim­ba, sasa, Lechantre huyo hapo.

Wakati mwingine kama ni kwa kuangalia pekee, unawe­za ukawa unaona kocha huyo Mfaransa huenda ni mkubwa kuliko Simba.

Huenda zaidi hadhi yake itaonekana kwa ubora wa kazi yake na kizuri ambacho mashabiki na wanachama wa Simba wanapaswa kuku­bali ubora wa kocha hauwezi kuanza kuonekana kwa siku moja au mbili, lazima muda unahita­jika.

Angalia mju­muiko wa benchi la ufundi, mako­cha watatu, mmo­ja wa Afrika ya Mashariki, mmoja Afrika Kaskazini na mwingine Ulaya. Hawa ni watu am­bao wanatakiwa ku­unganisha “Chem­istri” yao ili kufanya k a z i kwa umoja.

Muunganiko huo unatak­iwa pia kuunganisha hiyo “Chemistri” ili kufanya kazi na wachezaji vizuri, waelewane na kufanya kitu kwa pamoja na umoja.

Zingatia kuna suala la lugha ambalo Simba wamepata kama bahati ni kwamba, ma­kocha wote watatu wanazun­gumza Kifaransa kwa Ufasaha kwa kuwa nchi zote tatu zina­tumia lugha hiyo moja, yaani Ufaransa wenyewe, Tunisia na Burundi.

Lazima kuwe na subira ka­tika mabadiliko huwa kuna matatizo. Tuliona muda mch­ache wa mabadiliko ya Kocha Djuma, wako tayari walianza kulalama na kusema ana­wachanganya afukuzwe.

Baada ya mambo kukaa sawa na kuanza kuzinyan­yasa timu nyingine, wale­wale wakageuka na kuanza kumpongeza. Kweli hii ni tabia ya mashabiki wengi lakini ku­jitambua zaidi ya hapo, ni jam­bo zuri zaidi.

Kama mashabiki wataanza papara mapema hasa kama katika ubadilishaji wa mambo Lechantre atakuwa ameko­sea jambo, basi ujue watam­changanya zaidi na mwisho ataonekana hana lolote na kuondoka mapema.

Kikubwa ni kocha huyo ku­hakikisha naye anakuwa ma­kini katika mabadiliko yake ili kuhakikisha Simba inakwenda kwa mwendo wake ilionao kwa sasa.

Comments are closed.