The House of Favourite Newspapers

OKWI: MECHI NA WAARABU ILININYIMA USINGIZI

STRAIKA kiwembe wa Simba, raia wa Uganda, Emmanuel Okwi, amesema kuwa tangu mechi yao imalizike, hajapata usingizi mzuri kutokana na mawazo na namna alivyokuwa akiitafakari mechi hiyo.

 

Simba walikuwa ugenini nchini Misri kwa ajili ya kucheza na wenyeji wao Al Masry katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa katika Jiji la Port Said, ambapo Simba walitoka su­luhu. Hata hivyo, kikosi hicho kimeondoshwa katika mashindano hayo kufuatia sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa mkondo wa kwanza.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Okwi alisema kwamba mchezo huo ulikuwa mgumu lakini hakufurahishwa na matokeo waliyoyapata maana wali­pambana sana ili kushinda lakini mwisho wakapata ma­tokeo hayo ya kutofungana.

 

“Nimeumia sana kuona tunaondoshwa kwenye mashindano muhimu kama yale, mimi binafsi sikutegemea kutofaulu ila kwa kuwa mchezo wa mpira ndivyo ulivyo basi tumekubali kwani siku nyingine tutajipanga zaidi.

 

“Al Masry ni timu kubwa tunaiheshimu lakini kwa namna ambavyo tume­pigana, kama kusingekuwa na matatizo ya refa kutubania, naamini leo hii tungekuwa tutaongea mambo mengine,” alisema Okwi mwenye mabao 16 katika ligi kuu.

Musa Mateja,  Port Said.

Comments are closed.