The House of Favourite Newspapers

Waziri Mwakyembe Akutana na Uongozi wa Basketball Federation

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe (kulia) akiongea na uongozi wa Tanzania Basketball Federation (TBF) ukiongozwa na Rais wake Ndg. Phares Magesa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe leo amekutana na uongozi wa Tanzania Basketball Federation (TBF) ukiongozwa na Rais wake Ndg. Phares Magesa, katika mazungumzo hayo Mhe. Waziri ameupongeza uongozi mpya wa TBF kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuahidi kushirikiana na TBF kuhakikisha mchezo wa kikapu unachezwa kila sehemu.
Pia Mhe. Waziri ameahidi kushirikiana na TBF kutafuta wafadhili ndani na nje ya nchi ili kusaidia utekelezaji wa mpango mkakati wa TBF ambao unahusu kuendeleza mchezo kuanzia ngazi ya nchini, mchezo uanze kuchezwa kuanzia shule za msingi na mitaani kote, kujenga viwanja vipya vyenye hadhi ya kucheza michezo ya Kimataifa na kukarabati vya zamani ikiwemo uwanja wa ndani wa Taifa, kuhakikisha timu zetu zinashiriki mashindano ya ndani na nje ikiwemo kuhakikisha mashindano ya FIBA Zone V U 18 yatakayofanyika June 2018 na FIBA Zone V Club Championship October 2018 yanafanyika kwa mafanikio nchini, pia Mhe.
Waziri ametaka mashindano ya ndani ikiwemo Ligi za mikoa , ligi ya Taifa , Kombe la Taifa na la Muungano yaimarishwe na kuomba wafadhili zaidi wajitokeze kudhamini mashindano haya, Mhe. Waziri alieleza kufurahishwa na mchezo wa kikapu jinsi ulivyoshirkishi na navyopendwa na wanawake na wanaume na kuitangaza vizuri nchi yetu, na alifurahishwa sana alipokuwa kwenye ziara mkoani Mbeya kuona mchezo unachezwa kwa ari na hamasa kubwa na kuitaka mikoa na wilaya zote nchini ziige mifano ya mikoa inayofanya vizuri ikiwemo DSM, Mbeya , Dodoma, Mwanza , Arusha n.k. Aidha Mhe.
Waziri ameahidi kusaidia vyama vya michezo ikiwemo TBF kupata ofisi za kudumu za kufanyia shughuli zake ikiwa ni pamoja na kuwa tayari kushiriki katika harambee ya Kitaifa itakayoandaliwa kuchangia maendeleo ya kikapu nchini. Waziri ameahidi kuandaa kikao kingine na wataalamu wa Wizara yake ili kupanga mikakati zaidi na kufuatilia utekelezaji wa haya yaliyojadiliwa. Kikao hicho na Waziri kilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais wa TBF Ndg. Mboka Mwambusi.

Comments are closed.