The House of Favourite Newspapers

Serikali Yawasamehe Roma Mkatoliki na PretyKind, Wafutiwa Adhabu

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na Naibu wake, Juliana Shonza (katikati mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii hao baada ya kuongea na wanahabari.

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na Naibu wake, Juliana Shonza, leo wametangaza kufuta adhabu ya kufungia wasanii wa  muziki wa Kizazi Kipya, Roma Mkatoliki na Suzan Michael maarufu kama Pretykind.

Akizungumzia hilo, Waziri Mwakyembe alisema kuwa muda wowote kuanzia sasa Roma Mkatoliki atakuwa huru kufanya shughuli zake za muziki kama ilivyokuwa awali kwa sharti moja la kukamilisha taratibu za kujisajili BASATA.

Roma Mkatoliki ameviomba vyombo vya habari kutocheza wimbo wake wa Kibamia.

Mwanzoni mwa mwezi Machi, mwaka huu, serikali kupitia Wizara ya Habari ilitangaza kumfungia miezi sita msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na masuala ya muziki kwa kukaidi amri ya kubadilisha baadhi ya mashairi ya wimbo wake wa Kiba100.

Naibu Waziri, Juliana Shonza akiwa na Suzan Michael ‘Pretykind’. 

Suzan Michael maarufu kama Pretykind naye alipewa nafasi ya kuongea na wanahabari ambapo alitoa pongei kwa serikali kwa kumfundisha malezi mema na kuwaasa wasanii wenzake kuwa na tabia nzuri.

Comments are closed.