The House of Favourite Newspapers

Wenger Yupo ‘Siriazi’ Europa

BAADA ya kushinda mabao 4-1 dhidi ya CSKA Moscow katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya Europa League, Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema yupo makini na anachokifanya.

 

Usiku wa kuamkia jana kwenye Uwanja wa Emirates, Arsenal ilipata ushindi huo kwa mabao ya Aaron Ramsey (mawili dakika ya tisa na 28) na Alexandre Lacazette aliyefunga mabao mawili pia dakika ya 23 kwa penalti na 35.

Bao la CSKA lilifungwa na Aleksandr Golovin dakika ya 15. Wenger alisema: “Nipo makini na michuano hii naichukulia ‘siriazi’, tumeshinda dhidi ya timu nzuri, kazi tutaimaliza katika marudiano.”

Comments are closed.