The House of Favourite Newspapers

Yanga Yakwea Pipa, Saba Wagomea Safari -Video

Wachezaji wa timu ya Yanga.

KIKOSI cha Yanga kimeondoka kwenda nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Af­rika dhidi ya wapinzani wao, USM Alger huku wachezaji saba wakid­aiwa kugomea safari hiyo.

 

Yanga ambayo iliondoka jana Alhamisi, inatarajiwa kuvaana na Alger katika mchezo wa Kundi D utakao­pigwa keshokutwa Jumapili, wakiwa kundi moja na timu za Rayon Sport ya Rwanda na Gor Mahia ya nchini Kenya.

 

Wachezaji hao waliobaki jijini Dar ni Kelvin Yondani, Ibrahim Ajibu, Papy Kabam­ba Tshishimbi, Thabani Kamusoko, Beno Kakolan­ya, Obrey Chirwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Kikosi cha timu ya Yanga.

Akizungumza na Champi­oni Ijumaa, kocha mpya wa timu hiyo raia wa DR Congo, Zahera Mwinyi, alisema wachezaji hao wamebaki Dar na sababu kubwa ni madai ya malipo ya mishahara ya miezi mitatu wanayodai.

 

Zahera alisema aliona dalili za mgomo wa sa­fari hiyo siku mbili zilizopita baada ya wachezaji hao kugomea mazoezi yaliyofan­yika kwenye Chuo cha Polisi, Kurasini, Dar wakiwa katika maandalizi ya mchezo huo.

 

Aliongeza kuwa, licha ya kukosekana kwa wachezaji hao, kocha huyo amewaa­hidi Wanayanga kwenda kupambana wakiwa na kikosi hicho walichosafiri nacho kwenda Algeria na kupata matokeo mazuri.

 

“Nilishangaa kumuona kipa (Youth Rostand) klabuni na kuwepo kwenye msafara wa timu yetu unaokwenda Algeria, kwani ni kati ya wachezaji walioshindwa kufanya mazoezi ya mwisho tukijiandaa na mechi hii, hivyo ninajisikia faraja.

 

“Niseme kuwa, licha ya wachezaji hao kugoma tunakwenda huko kucheza kwa tahadhari kwa maana ya kushambulia kwa tahad­hari huku tukijilinda kuhak­ikisha tunapata matokeo mazuri.

 

“Kikubwa mashabiki wa Yanga watuombee tunakwenda kupambana, na jambo la kushukuru tunaanzia ugenini katika mashindano hayo, hivyo tutajitahidi tunapambana na kupata matokeo mazuri,” alisema Zahera.

 

Kikosi kilichosafiri kwenda Algeria ni makipa; Rostand, Ramadhani Kabwili na mabeki wa pembeni ni Has­san Kessy, Juma Abdul, Hajji Mwinyi, Gadier Michael.

 

Mabeki wa kati; Andrew Vincent ‘Dante’, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na viungo ni Said Makapu, Raphael Daudi, Pius Buswita.

 

Washambuliaji ni Yussuf Mhilu, Juma Mahadhi na Yo­hana Nkomola na mawinga ni Emmanuel Martin na Geofrey Mwashiuya.

Comments are closed.