The House of Favourite Newspapers

MWENDOKASI WASITISHWA

KAMPUNI inayotoa huduma katika mradi wa usafiei wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imsitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia leo saa 6:00 mchana kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la Jangwani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam.

 

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano UDART, Deus Bugaywa ambaye amesema UDART wameamua hayo kutokana na maji mengi ya mvua kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria pamoja na vyombo vya usafirishaji.

“Huduma zinatolewa kwa njia za Mbezi – Kimara, Kimara – Morroco, Kimara – Magomeni Mapipa, Kivukoni – Muhimbili, Gerezani – Kvukoni na Gerezani – Muhimbili. Huduma kamili zitarejea mara baada ya barabara kufunguliwa”, amesema Bugaywa.

Aidha, Bugaywa amewaomba radhi wananchi wanaotumia usafiri huo kwa usumbufu ambao utajitokeza kwa namna moja ama nyingine.

Comments are closed.